SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 29, 2014

HABARI KAMILI KUHUSU TUKIO LA MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEJINYONGA GUEST

Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.

MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,masainyotambofu.com ilipofatilia tukio hilo ilifanikiwa kuongea na mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya
mwisho kabla ya kujinyonga huku filamu yake ya kwanza ikiwa bado haijatoka na kuingia sokoni yenye jina la CHOZI.


Msanii huyo aliyetambulika kwa jina la usanii Koba aliiambia Website ya masainyotambofu.com kwamba siku moja kabla ya tukio Victor alifanya nao Shuting ya filamu iliotambulika kwa jina OUR FAMILYambayo ilikuwa ndio filamu ya marehemu Vicktor ya pili tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie,

MSEMAJI
Cha kushangaza ni kwamba filamu hiyo muhusika mkuu alikuwa ni marehemu Vicktor na katika filamu hiyo alicheza kwamba kuna msiba baba yake kafa na yeye mwenyewe mwisho wa filamu Picha yake hiyo mnayoiona hapo juu ilipigwa Ex na muhusika aliyecheza kama mdogo wake, Matokeo yake alivyomaliza kushut aliondoka na wasanii kadhaa wakaelekea katika ATM iliokwepo maeneo ya mjini kutoa hela ili awalipe wasanii walihusika katika kazi yake,

KABLA YA TUKIO
Kwa bahati mbaya ATM machine ikagomagoma kwa tatizo kidogo la kimtandao katika kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa na kuonekana hayuko sawa, Basi kwa bahati nzuri baada ya mda mchache ATM ilikaa vizuri na yeye mwenyewe ile hali ikatulia akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani huko mkoani Tanga,
Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo.

UCHUNGUZI
Kufika Bombo akapimwa kila kitu na kukutwa mzima hana tatizo lolote lile ikabidi warudi Gest walikofikia huko maeneo ya Kisosora, Marehemu akawalipa wasanii wote na kuwauliza kuwa kuna mtu anaemdai? Wakamjibu hakuna. Kila msanii akaingia chumbani kwake na kuendelea na zake, Kwa wakati ule marehemu aliingia chumbani kwake na kwakuwa ni Self Contain si rahisi kumuona mtu akitoka nje hovyo hovyo.

TUKIO
Asubuhi yakuamkia jumanne 28/01/2014 Wasanii wenzake walimgongea mlango wakaona kimya wakapatwa na wasiwasi ikabidi wamuite mwenye Gest na kusimulia hali halisi mwenye Gest akachukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mwenye kiti wa Serikali za mitaa mwenye kiti akatoa taarifa Polisi, Gari ya Polisi ikatia timu katika eneo la tukio na kuvunja mlango wakakuta mwili wa marehemu Victor ukiwa umening'inia kama unavyoonekana hapo pichani alitumia mkanda wake mwenyewe wa kiunoni kujinyongea. Vicktor kajinyonga na kuiaga dunia.
MWILI WA MAREHEMU
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali kuu ya mkoa wa Tanga Bombo. Marehemu ni mkazi wa mwanza na ameacha mke na mtoto mmoja, Mpaka sasa baadhi ya ndugu wa marehemu tayari wameshafika na wengine wanatarajiwa kufika kesho wa taratibu za kusafirisha mwili kwa maziko. 'Alisema Koba'

 MAREHEMU Vicktor baada ya kujinyonga

Marehemu Victor Enzi za uhai wake akiwa location
MWILI wa marehemu Victor ukitolewa Safari Juniour Gest kisosora.
MWILI wa marehemu Victor ukipakizwa kwenye Gari ya polisi.
Baadhi ya wananchi wakishangaashangaa katika eneo la tukio.
MWILI wa marehemu Victor baada ya kupakiwa kwenye Gari la Polisi.
CREDIT MASAINYOTAMBOFU.COM
MSANII WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA KWA KUJINYONGA 

clip_image001
MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR  ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,
Chanzo cha habari kiliieleza kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushoot filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwakujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika.
Ndugu msomaji taarifa kamili na picha za tukio zima la kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka Hospitali na mengineyo fatilia hapa utayapata hivi punde.
SOURCE:: MASAI NYOTAMBOFU

0 comments:

Post a Comment