Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi (mbele ya basi lililopinduka
aliyenyoosha mkono) akiangalia basi la Shabiby lililopinduka eneo la
kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.Basi hilo ambalo lilijeruhi abiria
28 akiwemo kondakta aliyevunjika miguu yote, lilipinduka katika
harakati zake za kulipita basi jingine.
Lori la mafuta lililogongwa na basi la Shabiby na kusababisha abiria 28 kujeruhiwa.
Kondakta wa basi la shabiby Tadei Mhando aliyevunjika miguu yote miwili baada ya basi hilo kupinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Waauguzi wa hospitali ya mkoa mjini hapa,wakimpeleka kondakta Tadei Mhando chumba cha upasuaji.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
ABIRIA
48 wa basi la kampuni ya Shabiby lifanyalo safari zake kati ya mkoa wa
Arusha na Dodoma, wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka wakati
likijaribu kupita basi jingine.
Basi
hilo aina ya Yutong lenye namba za usajili T.930 BUW, limepinduka
katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki Manispaa
ya Singida.
Ajali hiyo imetokea Januari 13 mwaka huu saa saba mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Arusha kuelekea mjini Dodoma.
Kondakta
wa basi hilo,Tadei Mhando amesema kati ya abiria hao,28 wakiwemo watoto
wawili,wamepata majeraha katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.
“Mimi
ndiye niliyeumia zaidi kuliko majeruhi wote wa basi letu.Nimevunjika
miguu yote miwili na sasa natarajia kuingizwa ‘theater’ kwa matibabu
zaidi.Tunashukuru hakuna mtu aliyepoteza maisha”,amesema Tadei.
Akifafanua
zaidi juu ya ajali hiyo,Tadei amesema walipofika eneo la tukio la
Kisaki ambalo lina mwiinuko huku basi lao likiwa kwenye mwendo
kasi,dereva wao alijaribu kulipita basi la princess Muna.
Amesema
katika jaribio hilo,mabasi yote mawili yakawa kwenye mwendo kasi
unaofanana na wakati huo huo,lori la mafuta lililokuwa linapishana na
mabasi hayo,liliibana basi la shabiby na kusababisha ligonge lori hilo
ubavuni karibu na kichwa.
“Kutokana
na kubanwa huko huku Shabiby likiwa kwenye mwendo kasi,dereva
alishindwa kulimudu na hivyo kusababisha lipinduke na kuharibika
vibaya”,alifafanua Tadei.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na kamati yake ya ulinzi, ilifika
hospital ya mkoa na kuwapa pole na majeruhi na kisha alienda eneo la
tukio Kisaki.
0 comments:
Post a Comment