Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amesema anawaachia Watanzania waamue mkweli kati ya kamati yake na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.Kauli hiyo ya Lembeli inafuatia taarifa ya gazeti moja la kila siku (Siyo Mwananchi), iliyomnukuu Nyalandu akisema ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyowang'oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.
Nyalandu anadaiwa kutoa kauli hiyo alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma na Manyara kuhusu mgogoro wa mipaka kati wanavijiji na Hifadhi ya Tarangire.
Pia, mgogoro huo unahusisha Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani.
Nyalandu alikaririwa akisema kutokana na taarifa hiyo kueleza wapo watu waliobakwa wakati siyo kweli. Tanzania imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora kutokana na ukiukwaji haki za binadamu.
Hata hivyo, Lembeli alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na kauli hiyo alijibu: "Sijaisoma hiyo habari ila nimeisikia tu, kama ni kweli ametoa kauli hiyo (Nyalandu) basi ni hatari."
Lembeli alisema anawaachia Watanzania kupima mkweli kati yake, kamati yake na Waziri Nyalandu katika jambo hilo.(P.T)
"Kwa sasa niko kijijini kwangu huku jimboni, lakini nitafafanua zaidi nitakaporejea Dar es Salaam," alisema.
Ripoti hiyo ya kamati ndogo ya
uchunguzi iliyoongozwa na Lembeli ndiyo iliyosababisha mawaziri wanne
kuwajibika, kutokana na kuibuliwa kwa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa
haki za binadamu. Mawaziri waliong'olewa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk
Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Dk Mathato David na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki alijiuzulu kabla.
Atangaza ubabe
Lembeli alikazia kwa kusema hawezi
kuishi kwa kuhofia vitisho vya maisha, kwa madai ya taarifa yake ya
Operesheni Tokomeza Ujangili iliyosababisha kung'olewa kwa mawaziri
wanne.
Akihutubia mkutano wa hadhara Kata ya Igunda, Lembeli alisema haogopi vitisho hivyo na ataendelea kutetea masihali ya umma.
Awali, Diwani wa kata hiyo, Tabu
Katoto wakati akimkaribisha, alimpa pole mbunge huyo kwa kazi ngumu na
lawama aliyoifanya mwaka jana kwa faida ya taifa, hali ambayo Lembeli
alisema inampa wakati mgumu kutokana na watu wenye akili ndogo kumpa
vitisho. vya maisha yake.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment