Daladala likiwaka moto huku kikosi cha zimamoto na uokoaji wakizima moto huo |
Gari la Zimamoto na uokoaji mjini Iringa likizima moto uliokuwa ukiteketeza daladala eneo la Samora leo |
Hili ni basi ambalo pia limewaka upande wa mbe |
Konda wa daladala hilo akiwa na kifaa cha kuzimia moto ambacho kimenusurika katika moto huo |
Mmoja kati ya askari wa Zima moto mjini Iringa akilitazama daladala hilo |
Hivi ndivyo moto huo ulivyoteketeza daladala hilo |
Askari wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji mjini Iringa Bw JOhn Zacharia akikagua kifaa cha kuzimia moto ambacho kilikutwa kikiwa kibovu na si msaada kwao |
Bw Filibert Mwihava akizungumza na mtandao huu |
Huyu ni mmoja kati ya mafundi wazoefu ambao walikuwa wamewaachia wanafunzi hao kazi |
Na Francis Godwin
BASI
mmoja lanusurika kuwaka moto na daladala moja yateketea yote kwa
moto wakati wanafunzi wa masomo ya kuunga vyuma katika gereji bubu
eneo la uwanja wa Samora mjini Iringa wakijifunza kuunga ngao ya
daladala hiyo yenye namba za usajili T189 AWN .
Tukio
hilo limetokea leo majira ya 2.15 mchana wakati vijana wawili
wanaojifunza kuunga wakiendelea na mafunzo ya kuunga ngao ya
daladala hilo.
Akizungumzia
ajali hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa gereji hiyo Filibert
Mwihava alisema kuwa chanzo cha daladala hilo kuwaka moto ni
vijana wawili ambao wanajifunza ufundi wa kuunga vyuma katika eneo
hilo kufanya kazi hiyo bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo.
Kwani
alisema vijana hao walikuwa wakiunga ngao ya nyuma ya daladala
hilo jirani na tenki la mafuta na kutokana na cheche zilizokuwa
zikitoka zilisababisha moto kuibuka kwa kasi .
Hata
hivyo alisema mbali ya kuwa na kifaa cha kuzimia moto bado
walishindwa kukitumia kifaa hicho kutokana na kutokuwa na elimu ya
kutosha ya kukitumia.
Mwihava
alisema kutokana na moto huo kushika daladala hilo linalofanya
safari zake kati ya Tumaini na Zizi la Ng'ombe mjini Iringa hakuna
mtu aliyezulika zaidi ya basi lenye namba za usajili T 457 AMQ
kutetekea upande wa mbele kabla ya kuokolewa .
Pia
alishukuru kikosi cha zimamoto na uokoaji mjini Iringa ambao
walifika kwa wakati na kufanikiwa kuzima moto huo ambao ungeweza
kusababisha madhara makubwa katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na
ofisi maduka ya watu waliojenga kuzunguka uwanja wa Samora
kuteketea..
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kiongozi wa askari wa zimamoto ambao
walifika eneo hilo John Zacharia alisema kuwa kuwa chanzo cha moto
huo ni uzembe wa ofisi hiyo.
Kwani alisema hata kifaa cha zimamoto walichokuwa nacho kilikuwa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika muda mrefu.
Huku
kifaa cha kuzimia moto kilichokuwemo katika daladala hilo ni kifaa
ambacho kidogo zaidi na maalum kwa gari dogo ambacho pia kilikuwa
hakifanyi kazi.
Zacharia
aliwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuzingatia sheria za
zimamoto ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto badala ya kudanganya na
kuona kama wanaonewa pale wanapolazimishwa kuwa na vifaa hivyo.
|
0 comments:
Post a Comment