SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, December 12, 2013

Yasin Saleh bingwa wa gofu michuano ya NSSF,ORYX Tanzania open

Wachezaji wa gofu wa kulipwa walioshiriki mashindano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mashindano hayo kwa upande wa Profesionals ambao ni ORYX Energies Ltd.Mwenye t-shirt nyekundu kwa waliochuchumaa ni mkurugenzi wa kampuni ya Oryx,Chris Swat na aliyesimama mwenye t-shirt nyekundu ni mwakilishi wa mauozo wa kampuni ya Oryx kanda ya kaskazini Edga Mhagama.
Wacheza wa gofu wa ridhaa walioshiriki mashindano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mashindano hayo kwa upande wa Armature ambao ni shirika la hifadhi ya jamii la NSSF.
Baadhi ya maofisa kutoka NSSF mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washindi katika mashindano ya gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013.
Afisa mtndaji utawala wa kiwanda cha sukai cha TPC akizungumza jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa michuano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya TPC.
Afisa operesheni wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa Kilimanjaro Daudi Mwangole akizungumza jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa michuano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya TPC.
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa akimwakilsiha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama katika utoaji wa zawadi kwa washindi wa michuano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya TPC.
Mkurugenzi wa kampuni ya ORYX,Chris Swat akifurahia jambo na mshindi wa mashindano ya gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 kwa upande wa wachezaji wa kulipwa Yasin Saleh.
Mkurugenzi wa kampuni ya ORYX,Chris Swat akikabidhi zawadi ya jiko pamoja na mtungi wa gesi kwa mmoja washiriki wa michuano ya gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 waliofanya vizuri kwa wenye umri juu ya miaka 55.Vicent Maguu.
Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa ridhaa katika mashindano ya gofu ya NSSF,ORYX Tanzania 2013,Frank Roman akikabidhiwa kikombe na katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa,katikati ni mwakilishi wa wadhamini wa mashindano hayo NSSF,Daudi Mwangole.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

MASHINDANO makubwa ya mchezo wa Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open yamemalizika juzi katika viwanja vya TPC mkoani Kilimanjaro huku ikishudiwa mchezaji Yasin Salehe wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana akishika nafasi ya kwanza kwa upande wa wachezaji wa kulipwa baada ya kupiga mikwaju 302.

Saleh alifanikiwa kujinyakulia kitita cha fedha kilichotolewa na kampuni ya ORYX ambao ndio walikuwa wadhamini kwa upande wa wachezaji wa kulipwa baada ya kuwabwaga wapinzani wake Godfrey Revelian aliyepiga mikwaju 303 na Hassani Kadio aliyeshika nafasi ya tatu kwa kupiga mikwaju 308.

Nafasi ya nne kwa upande wa wachezaji wa kulipwa ilichukuliwa na mchezaji John Davies wa klabu ya gofu ya Mombasa baada ya kupiga mikwaju 309 huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Salim Dilunga aliyepiga mikwaju 310 na nafasi ya sita kwa washindi walipewa zawadi ni Salim Mwanyenza aliyepiga mikwaju 312.

Upande wa wachezaji wa gofu wa ridhaa waliodhaminiwa na mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF,mshindi wa kwanza alikuwa ni Frank Roman aliyepiga mikwaju 293 akifungana na mpinzani wake Ally Mcharo aliyeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mchezaji Nuru Morel aliyepiga mikwaju 294.

Wasindi wengine na mikwaju waliyopigwa kwenye mabano ni Abas Adam(297) aliyeshika nafasi ya nne,Abdala Yusuph (301)aliyeshika nafasi ya tano huku Jimmy Morel (306) akishika nafasi ya sita.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa alisema serikali mkoani Kilimanjaro itaendelea kusaidia michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa gofu ili kuweza kupata wachezaji watakao wakilisha taifa katika mashindano mbalimbali.

“Rai yangu ni kwamba tusifikirie kuanza kucheza mchezo huu wa gofu tukiwa ukubwani…ni vema tukafikiria kuanza kuwalea vijana katika mchezo huu ambao wakifika umri mkubwa ni wazi watakuwa ni wachezaji wazuri na ambao watatuwakilisha vyema.”alisema Issa.

Alisema mkoa wa Kilimanjaro umeweka mikakati ya kurejesha hali ya michezo katika mkoa kwa kuundwa kamati maalumu ambayo itakuwa na wajibu wa kufanya vikao vya kuangalia miechezo inaendaje hasa kwa kushirikisha vyama vya michezo.

Naye katibu wa chama cha mchezo wa Gofu nchini (TGU)Mohamed Sadick aliipongeza kampuni ya TPC pamoja na wadhamini wa mashindano hayo shirika la hifadhi ya jamii NSSF pamoja na kampuni ya Oryx Energizer kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa ya gofu nchini.

“Suala la kushirikisha Professionals ni jema sana kwani wachezaji chipukizi wanajifunza kutoka kwao kwani tunajenga gofers wazuri ambao wanajua sheria na hili lazima tuendelee kulisisistza kila atakaye andaa mashindano ashirikishe pia Professionals ili kusaidia viwango vya vijana wetu”alisema Sadick.

Kwa upande wake afisa utawala wa kiwanda cha sukari TPC Jafary Ally alisema kampuni ya TPC imeendelea kufanya ukarabati wa maeneo mbalimbali ya uwanja wa gofu ili uweze kuwa na kiwango kinachotakiwa kimataifa.
NA ANKAL MICHUZI

0 comments:

Post a Comment