SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 24, 2013

MCHEZAJI WA BORA WA LIGI YA BRAZIL - EVERTON RIBEIRO ASEMA ATAICHAGUA MAN UNITED MBELE YA REAL MADRID

Kiungo wa kibrazil Everton Ribeiro kwa mara nyingine ameelezea matamanio ya kujiunga na klabu ya Manchester United.

United iliwatuma maskauti wake wa vipaji kwenda nchini Brazil kumuangalia staa huyo wa timu ya Cruzeiro na kocha David Moyes anafikiria kutuma ofa rasmi ya £12million ili kukamilisha usajili wa kiungo huyo, ambaye mwezi uliopita alishinda tuzo ya kuwa mwanasoka bora wa ligi ya Brazil.
Hata hiyo, United watakabiliana na upinzani kutka kwa Liverpool na Real Madrid ambao nao wamevutiwa na mchezaji huyo.
Ribeiro ambaye huko nyuma aliwahi kucheza katika mashindano ya vijana na United alipoulizwa na Globoesporte kama angependelea kujiunga na United badala ya Madrid, kiungo huyo mwenye miaka 24 alisema: ‘Ndio, ningependea kucheza United, mfumo ambao United wanaendesha timu ni bora kabisa duniani. Nimewahi kuwepo mahala pale na pia nilienda kupata mafunzo kutoka Alex Ferguson nilipokuwa kinda. ’
Wakala wa mchezaji huyo Robson Ferreira hivi karibuni alinukuliwa akisema: Manchester United wanamtaka Ribeiro,  David Moyes amevutiwa sana. Nilishaenda England na nikaongea rasmi na United.’


CHANZO NA SHAFFIH DAUDA

0 comments:

Post a Comment