SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, November 7, 2013

Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening ziarani nchini Tanzania

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akigonga kengele kuashiria kuanzishwa rasmi kwa ushirikiano mpya baina ya Tz na Soko la Hisa la London, akishuhudia ni Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, J. Greening.
  Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening akitoa hotuba yake.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma hotuba yake
Wakifatilia tukio kwa umakini, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose na Mkuu wa DFID, Marshall Elliott.
---
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa (UK’s Secretary of State for International Development (DFID)) Justine Greening wamedhamiria kuanzisha ushirikiano mpya na imara katika kuchochea biashara na maendeleo ya kiuchumi ili kuwanufaisha watanzania hasa walio katika lindi la umaskini.
Akizungumza katika tukio la pamoja la uzinduzi rasmi wa ushirikiano wa hali ya juu wa kiuchumi mnamo Novemba 5 jijini Dar es Salaam ambapo tutashuhudia Uingereza  na Tanzania ikiimarisha kwa ukaribu mahusiano ya kiuchumi, inategemewa ushirikiano huo utasaidia kuongeza kwa zaidi ya mara dufu idadi ya makampuni ya Uingereza ambayo yanafanya biashara nchini Tanzania hasa katika sekta ya nishati endelevu na kilimo ifikapo mwaka 2015. Tanzania ni miongoni mwa nchini tano za Afrika ambazo zimeingia makubaliano kama hayo na Uingereza, nyingine zikiwamo; Ghana, Msumbiji, Ivory Coast na Angola.
Waziri huyo wa Maendeleo ya Kimataifa ameambatana na ujumbe wa  wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wawakilishi wa juu kutoka katika mashirika 19 ya Uingereza na wafanyabiashara wa kimataifa wakitizama namna mpya ya kuchochea ajira na uwekezaji katika bara zima. Waziri huyu wa Maendeleo wa Uingereza anaitumia safari hii kutanganza ushirikiano mpya kati ya Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), biashara na kusaidia watu wa hali duni nchini Tanzania kunufaika na ukuaji wa kiuchumi. Uwekezaji utakuwa katika mfumo wa mkopo na si kama ilivyozoeleka katika mfumo wa misaada. Ni kwa mara ya kwanza dunia nzima  DFID kuandaa ujumbe kama huu wa kimataifa.
Justine Greening alisema: “Kwa muda mrefu sekta ya maendeleo imeona ujuzi na uwezo wa sekta binafsi katika juhudi tofauti na zile ambazo wao wanajihusisha. Nataka kuchukua mfumo tofauti.
 “Namna ya pekee kwa nchi zinazoendelea kusitisha utegemezi wao katika misaada ni kwa kutengeneza ajira zaidi, ukuaji na ukusanyaji kodi. Mwishowe, kazi ndiyo njia ya kipekee endelevu ya kumtoa mtu katika umaskini.
Biashara inaweza kuleta uwekezaji na ubunifu hasa unaohitajiwa katika kiwango ambacho kitakuwa cha mabadiliko. Uwekezaji wenye kuwajibika unatoa fursa za kiuchumi kwa jamii. Ni tija kwetu sisi kufanya kazi na wafanyabiashara kuhakikisha mipango yao inasaidia jamii ya kawaida.”
Justine Greening aanzisha jitihada mpya nne za eneo la kibiashara kusaidia watu maskini zaidi nchini Tanzania kunufaika na ukuaji wa kiuchumi:
  • Kufanya kazi na Unilever, the Wood Family Trust na Gatsby Foundation na kufata viwango na masharti yote yanayowekwa, DFID imeingia ubia kuwekeza katika mradi wa chai. Kutegemea na makubaliano ya mwisho baina ya wahusika, DFID itatoa mpaka Paundi 7.5 Milioni kuwezesha ubia kuwekeza katika mradi wa chai katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Ruzuku itasaidia kukuza kipato cha zaidi ya wakulima wa chai 3,600 ambao wapo zaidi ya vijiji 27. Ruzuku itarudishwa kwa uwekezaji unaofuata na Wood Family Trust.
  • Paundi 7.5 Milioni kwa The Wood Family Trust na Gatsby kuwekeza katika kiwanda kipya cha chai cha Uniliver kilichopo Njombe, Kusini Magharibi mwa Tanzania. Ruzuku itasaidia kipato kwa zaidi ya wakulima wa chai 3,600 waliosambaa katika vijiji 27. Ruzuku itarudishwa kwa uwekezaji unaofuata  na Wood Family Trust.
  • Paundi 3.3 milioni kwa shirika la Equity for Africa, taasisi ya Uingereza inayotoa ruzuku kwa wafanyabiashara wa kilimo wadogo na wa kati nchini Tanzania. Ruzuku ya DFID itawezesha Equity for Africa kutoa ruzuku zaidi kwa wafanyabiashara wa kilimo wadogo na wa kati kupata pembejeo za kilimo mkoani Mbeya. Kikawaida, wawekezaji wamekuwa wakisita kuwekeza katika hizi hatua za mwanzoni. Bila ushirikiano wa DFID katika kuwekeza, wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Mbeya wangeendelea kutaabika katika kupata mikopo.
  • Kufadhili ujenzi mpya wa kituo cha kufua umeme wa maji, kuchochea uzalishaji katika kiwanda cha Tanzania Tea Packers Ltd. DFID itatoa Paundi 2.5 Milioni kutia sahihi makubaliano na Shirika la Uzalishaji na Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO).
  • Paundi 6.7 Milioni kwa Kilombero Plantations Ltd (KPL), kinara wa uzalishaji wa mchele Afrika Mashariki, kusaidia kilimo cha mpunga. Miundo mbinu duni ya umma inarudisha nyuma kampuni. Ruzuku hii itasaidia biashara kuweza kushinda kikwazo cha miundombinu duni, kumwagilia sehemu kubwa zaidi ya ardhi na kuongeza mazao.  Tayari KPL inafanya kazi na wakulima wadogo wadogo zaidi ya 5,000 na inapanga kuongeza zaidi.
Greening pia alitangaza kuanzishwa kwa ushirikano mpya wa soko la hisa la London katika kuchochea masoko ya mitaji katika Afrika Mashariki. Awamu ya kwanza ya ushirikiano utatoa mafunzo kwa hadi wataalamu 20 wa kifedha, wasimamizi na maafisa wa kiserikali wa Afrika Mashariki katika Shule ya Soko la Hisa London.
Akiongea katika uzinduzi wa ushirikiano baina ya Uingereza na Tanzania katika Nyanja ya Uchumi Justine Greening alisema:
 “Kwa muda mrefu sekta ya misaada imekuwa ikiacha kuzingatia ujuzi na mchango wa sekta binafsi. Nataka kuchukua mfumo tofauti. Namna pekee kwa nchi zinazoendelea kusitisha utegemezi wao katika misaada ni kwa kutengeneza ajira zaidi na ukuaji. Hii ndiyo njia muafaka na endelevu kutoka nje ya umaskini”
Waziri Greening alitambua ukuaji mkubwa kiuchumi ambao Tanzania umepitia takribani asilimia 6 ndani ya muongo uliopita lakini bado asilimia 30 ya watu wake wanaishi chini ya Paundi 7 kwa mwezi.
 “Biashara zinaanza kukua na kupata faida”, alisema, “Makampuni ya Uingereza tayari yanaongoza katika kuwekeza Tanzania, kwa kuwa na takribani makampuni yaliyosajiliwa 35 yakifanya shughuli zake hapa nchini. Lakini bado mazingira duni ya kimiundo mbinu, ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi, mifumo migumu ya kikodi na changamoto zingine zinazozuia kufikia malengo yake makuu na uwezo wao”
Bi. Greening alisema, anaamini biashara zingeweza kuleta zaidi uwekezaji, kodi na ubunifu unaohitajiwa. Kwa wakati huo huo, utaalamu wa DFID na usaidizi unaweza kuchochea uwekezaji mpya na kutengeneza ajira mpya hasa katika sehemu za mazingira duni:
Nataka ubunifu huu pamoja na uwekezaji katika utengenezwaji wa ajira kuwa moja ya sehemu kubwa ya namna DFID itakavofafanya kazi siku za usoni. Naitizama Tanzania kama nchi yenye dalili njema linapokuja suala la mfumo mpya. Nina amini mambo ambayo yanafanya kazi hapa yanaweza kuigwa pia katika nchi nyingine ndani ya Afrika na pia kwa mataifa mengine yanayoendelea”.
-
Michael Dalali
Afisa Miradi na Mawasiliano
Ubalozi wa Uingereza
Dar es Salaam
Simu: +255 (0) 22 229 0269
Simu ya mkononi: +255 (0)762 791 991

0 comments:

Post a Comment