Afisa Habari wa
Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungmza na wanafunzi wa
shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro juu ya umuhimu wa kujihusisha na
kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa ziara za kutembelea shule mbalimbali za mkoa
huo.
=======
Na.
Mwandishi wetu.
Vijana
wa shule za sekondari nchini wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi watakapomaliza
masomo yao juu ya kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya milenia kwa sababu ni
dira ya maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Akizungumza
na wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari hivi
karibuni, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkhoma
Ledama amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote za maendelo kwa vijana
walio na wasio mashuleni.
Bi.
Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye kazi za kujitolea na kuhakikisha wanapeleka
elimu waliopata kupitia vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii na kuhamasisha
dhana ya kujitolea kwa maslahi ya nchi.
“kila
ndani ya saa moja tuna vijana 50 ambao wanapata maambukizi ya VVU kati ya miaka
14-24 ambao wengi kati ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe na masuala ya
mapenzi mnapokuwa mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.
Bi. Usia Nkhoma
Ledama akionyesha takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa hivi karibuni (“Young
People Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25 ya watoto wa kike chini ya
miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.
Pichani juu na
chini ni vijana wa shule ya Sekondari Umbwe wakifuatilia kwa umakini mjadala wa
masuala ya Umoja wa Mataifa uliiongozwa na Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo
pichani).
Mwenyekiti Taifa wa
Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab
Nasser akifafanua jambo kwa vijana waliojiunga na klabu za Umoja wa Mataifa
shuleni hapo juu ya umuhimu wa kuwa na cheti cha klabu ya Umoja wa
Mataifa
Msafara wa wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya
Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakitazama baadhi ya kazi mbalimbali
zinazofanywa na klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya sekondari Umbwe
ikiwemo shughuli za kuchangia damu, kusafisha mazingira na mengineyo
yajihusishayo moja kwa moja na shughuli za jamii.
"Ubovu wa
miundombinu ni changamoto kubwa kwa ziara yetu lakini ujumbe wa shughuli za
Umoja wa Mataifa lazima ziwafikie walengwa".
Afisa Habari wa
Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifurahia uwepo wake
mbele ya wanafunzi wa Kibosho Girls shule ambayo binafsi alisoma miaka 20
iliyopita, ambapo pia ujio wake ulikuwa chachu na hamasa kubwa kwa wanafunzi wa
shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi
wa shule ya Wasichana Kibosho wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkhoma
Ledama.
Afisa Habari wa
Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwasisitizia wasichana
wa shule ya Kibosho juu ya umuhimu wa kujiamini na kujitambua wakati wa maamuzi
yao binafsi.
Mmoja wa wanafunzi
akiuliza swali kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa.
Kwa picha zaidi
ingia
BOFAYAHAPA
0 comments:
Post a Comment