Mhe. Anne Makinda ( Mb)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika mkutano wa
mwaka unaowakutanisha maspika na wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani katika
mkutano wa siku mbili unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano
huu umeandaliwa kwa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Inter-Parliamentary
Union ( IPU) katika mkutano huu pamoja na mambo mengine wabunge wanajadiliana
na kubadilisha mawazo kuhusu nafasi wa mabunge katika majadilianao
yannayoendelea hivi sasa kuhusu ajenda mpaya za Maendeleo Endelevu baada ya
2015. Kulia kwa Mhe. Spika ni Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi
Maalum
Maspika wa Mabunge na wabunge kutoka zaidi ya nchi mia moja jana alhamis, wameanza mkutano wao wa mwaka wa siku mbili unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, ambao umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa kupitia Baraza lake la Uchumi na Maendeleo ( ECOSOC) na Inter- Parliamentary Union ( IPU) unaongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (Mb).
Mada kuu ya mkutano huu ni Re-thinking sustainable development: the quest for a ‘ transformational’ global agenda in 2015 ambapo wabunge wamekuwa wakijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mchango wa Mabunge katika maandalizi ya Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Mkutano umefunguliwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. John Ashe ambaye alitambua mchango wa mabunge na wabunge katika kusimamia siyo tu utendaji wa serikali, utungaji wa sheria na sera mbalimbali na ukusanyaji wa mapato bali pia katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya wananchi. Akiwahimiza kuchagiza na kuhimiza maandalizi ya ajenda mpya za malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Wengine waliozungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano ni Rais wa ECOSOC Bw Nestor Osorio na Rais wa IPU Bw. Abdelwahadi Radi
Aidha wabunge katika siku ya kwanza ya mkutano wao pia wamejadiliana na kubasilishana mawazo na uzoefu katika mada inayohusu ‘ Jinsia kama kitovu cha maendeleo,namna ya kuunda malengo mapya’. Mkazo ukiwa katika kuhimiza ushiriki wa wanawake, vijana na asasi za kiraia
Katika siku ya pili ya mkutano utakofanyika siku ya ijumaa, Mhe, Spika Anne Makinda ( Mb) atakuwa mmoja wa wanajopo katika mada itakayokuwa inazungumzia utawala wa kidemokrasia na nafasi yake katika Maendeleo endelevu.
Washiriki wengine katika jopo hilo watakuwa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson, Balozi wa Usiswi katika Umoja wa Mataifa, Bw. Paul Seger na Balozi wa Costa Rica, Bw. Eduardo Ulibarri.

0 comments:
Post a Comment