SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 15, 2013

Ronaldo akiwa katika picha ya pamoja na bale 

Madrid, Hispania. Winga wa Real Madrid, Gareth Bale ameanza kuonyesha cheche zake Hispania na leo atakiongoza kikosi cha Carlo Ancelotti kuivaa Real Sociedad.
 
Winga huyo wa Wales alianza kuonyesha makali yake katika Ligi ya Mabingwa tangu aliposajiliwa kwa pauni 76.4 milioni Septemba, Jumatano alifunga bao moja wakati Madrid ilipotoka sare 2-2 na Juventus na kuwahakikishia vigogo hao wa Hispania kucheza 16 bora.
 
Bale pia alifunga mabao mawili na kutegeneza manne kwa Real katika mechi zake mbili dhidi ya Sevilla na Rayo Vallecano, ushirikiano wake na Cristiano Ronaldo, Karim Benzema umeanza kuwa mwiba mkali kwa timu pinzani.
 
Ronaldo ambaye pia alifunga Turin na kumfanya kufikisha rekodi ya kufunga mabao 222 katika mechi 215 alizocheza Madrid.
 
Ronaldo, Bale na Benzema wanategemea kuanza pamoja mbele, huku Sergio Ramos akiwa nje katika kikosi cha Ancelotti, lakini pengo hilo linaweza kuzibwa na Dani Carvajal au Alvaro Arbeloa.
 
Real wanaweza kupunguza tofauti ya pointi na kubaki tatu kwa Barca na mbili kwa Atletico Madrid kabla ya mechi zao kesho.
 
Vijana wa Catalans watawafuta Real Betis huku wakiwa wameimalika zaidi baada ya Lionel Messi, kuanza kuzifumania nyavu na Jumatano alifunga bao mbili waliposhinda 3-1 dhidi AC Milan katika Ligi ya Mabingwa.
 
Messi hajafunga bao lolote katika mechi nne za La Liga ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mwili kupita.
 
Mechi nyingine ya kuvutia wiki hii itawashudia Atletico wakiwavaa Villarreal.Atletico imefuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Austria Vienna huku Diego Costa akipachika bao lake la 16 msimu huu.
 

0 comments:

Post a Comment