SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 31, 2013

WARSHA YA MAFUNZO KUHUSU KUENEA KWA HAKI YA JANGWA,UKAME NA MAENDELEO ENDELEVU YA ARDHI YAFUNGULIWA MJINI BAGAMMOYO LEO

 
  Kaimu Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais bibi  Magdalena Mtenga akimkaribisha mgeni Rasmi Injinia Angelina  Madete aweze kufungua warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa   haki ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini  Bagamoyo
Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina  Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka  sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu  kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo leo. 
 Sehemu ya wajumbe wa warsha ya  mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini  Bagamoyo wakiskliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete. 
 Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya  jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini  Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi  katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete.
 
 *****
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia  Angelina Madete  amesema ukame umekuwa tatizo kubwa sana katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania. Na pia umeleta athari sana katika swala zima la mazingira, ameongeza   kuwa katika Africa inakadiriwa aslimia 73 ya nchi imepunguza uwezo wa kuzalisha chakula na hii imepelekea kuongezeka kwa ukame  na hivyo kupelekea upungufu wa chakula Nchini.   

Alitaja baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga,Mara, Iringa, Manyara na Arusha.  Amesema hayo leo mjini Bagamoyo  wakati wa  ufunguzi wa warsha ya  siku mbili kuhusu  juu ya   kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo endelevu ya ardhi. 

Warsha hiyo  imewashhirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo  kuepuka  janga la ukame. Akiongea katika warsha hiyo Injinia Madete alisema  kuwa ukame unaleta umaskini na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda sehemu zingine zisizo na ukame. 

Aliendelea kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame(United Nations Convetion to Combat Dessertification UNCCD)  na pia serikali inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame(Nationala Action Programme to Combat Dessertification-NAP). Na kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.

Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa (UNDP)
NA ANKA MICHUZI
.

0 comments:

Post a Comment