Mkuu
wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Bi.Herieth Koka(kushoto)akimpatia
mmoja wa wateja keki aliefika dukani hapo ikiwa ni ishara ya kuendelea
kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimfanyia mahojiano
Afisa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom
Tanzania,Bi.Herieth Lwakatare,kuhusiana na kuadhimisha wiki ya huduma
kwa wateja nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza akisalimiana na baadhi ya
wateja waliofika kupata huduma mbalimbali Vodashop Mlimani City na
kupata frusa ya kujumwika na Mkurugenzi huyo katika kusherehekea na
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Afisa
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.Herieth
Lwakatare(katikati)akipozi kwa picha na wafanyakazi wenzake.
Mkuu
wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen
akiwafafanulia jambo baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya
waliotembelea makao makuu katika kusherehekea na kuadhimisha wiki ya
huduma kwa wateja nchini.
Washindi
wa zawadi ya huduma bora kwa wateja wa ndani waliochaguliwa na Idara ya
Mahusianao na Mawasiliano na Idara ya Wateja wa Mikataba Zenobius Mlowe
(kulia) kutoka idara ya manunuzi na Faraji Hiza(kulia) wa idara ya
Huduma kwa Wateja wakiwa na tuzo zao katika picha ya pamoja na wasanii
wa kike wa kizazi kipya mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao katika hafla
fupi iliyofanyika kwenye idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Vodacom
Makao Makuu.
Meneja
wa Mradi wa MWEI Bi.Grace Lyon kushoto aliesimama akiwa amepozi kwa
picha na baadhi ya wasanii wakike wa kizazi kipya waliotembelea makao
makuu ya Vodacom katika kusherehesha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
====
====
Kampuni
ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wiki hii inaungana na dunia nzima
katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Maadhimisho hayo ambayo yalianza mnamo tarehe 7 yanaendelea mpaka
tarehe 11 ya mwezi huu yakiambatana na shughuli mbalimbali ambazo
zikifanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika jamii ambao wataendelea
kujumuika pamoja na wateja wao sehemu mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Makao makuu ya kampuni hiyo
yaliyopo Mlimani City,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza, alisema Vodacom inayofuraha kubwa sana
kwa kuendelea kufurahishwa na kuungwa mkono na alitoa wito kwa
watanzania kuendelea kutumia huduma ya M-PESA kwani ni sehemu ya maisha
ya watanzania hivi sasa na kuwahakikishia kuwa kampuni yake itaendelea
kutoa huduma bora na za uhakika za mawasiliano hapa nchini.
Katika
ufunguzi huo, Meza kwa kushirikiana na wafanyakazi na baadhi ya wateja
kwa pamoja walikata keki kuashiria kuanza kwa wiki hii ambapo wateja
walipata kula pamoja. Vilevile zawadi mbalimbali ziligawiwa kama
shukrani kwa kuunga mkono na kuendelea kutumia mtandao wa Vodacom.
Kama
kampuni ushirikiano baina ya wateja na wafanyakazi ni jambo muhimu sana
kwani huwa ni wakati muwafaka wa kubadilishana mawazo kujua nini wateja
wanachokihitaji kiboreshwe na kupata majibu yaliyosahihi katika soko
hili lenye ushindani."Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele siku zote
sio tu katika kutoa huduma bora bali pia na kuwasikiliza wateja
wanataka kitu gani.
Hivyo
tungependa kuwaambia wateja wetu tunashukuru sana kwa kutuunga mkono kwa
kipindi chote hicho na pia kuendelea kutumia huduma zetu," Meza
alisema.
MA MICHUZI MATUKIO
MA MICHUZI MATUKIO
0 comments:
Post a Comment