SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 7, 2013

SHEREHE YA MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI 22 WA JESHI LA MAGEREZA WALIOPANDISHWA CHEO HICHO YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

  Mke wa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Flora Minja(wa kwanza kulia) akiwa katika hafla fupi ya kuwapongeza Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni. Sherehe za uvalishaji vyeo zimefanyika jana katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salam(wa kwanza kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Helmet Iniciative Company Ltd, Alpherio Moris ambaye pia ni Mtaalam Mshauri katika mradi  wa uzalishaji wa Kofia ngumu wa Gereza Kuu Ukonga.
  Baadhi ya Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifurahia katika hafla fupi ya kuwapongeza mara baada ya zoezi la uvalishaji wa cheo hicho kufanyika katika Viwanja vya Bwalo Kuu la Maafisa wa Mgereza, Ukonga Dar es Salaam(wa nne kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Gideon Nkana ambaye pia ni Mdhibiti Mkuu wa Fedha wa Jeshi la Magereza akifurahia kupandishwa cheo hicho na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Kikwete kama anavyoonekana
  Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiwa katika hafla ya kuwapongeza Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamepandishwa cheo hicho na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja( wa tatu kushoto) akiwa na Makamishna wa Magereza katika meza Kuu pamoja na Viongozi Wengine Waandamizi wa Serikali(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha,  Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dickson Maimu.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

0 comments:

Post a Comment