SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 8, 2013

Muendelezo wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Nchini Marekani Atembelea Chuo Kikuu Cha Tiba cha Alabama

 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod  Slaa akiongozwa na Professor ambaye pia ni dean msaidizi
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akielekezwa kwenye chumba cha Mikutano na rais wa chuo cha tiba
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa na Dean wakiwa kwenye maongezi ya kufanya kazi pamoja
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akipewa maelekezo na rais wa chuo cha Tiba
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa pamoja na viongozi wa Chuo cha Tiba
---
Akiwa anaendelea na ziara yake nchini Marekani, siku ya ijumaa katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilibrod Slaa alitembelea Chuo kikuu cha tiba cha Alabama ambako alilakiwa na viongozi wa juu wa chuo hicho
Chuo kikuu cha Alabama ina wanafunzi 16,000 katika Kitengo cha tiba. Hii ndio moja ya vyuo vikubwa nchini marekani katika maswala ya tiba, ikiwa na vitengo karibia vyote vinavyotibu magonjwa mbali mbali. Chuo hicho pia ufanya utafiti nchi nyingi duniani husasan afrika. Chuo hicho ushirikiana na nchi kama Afrika kusini, Zambia, Malawi, na Aljeria katika mambo ya utafiti na kutayarisha watafiti. Kadhalika imekuwa ikisaidia mataifa kama Saudi Arabia, Uchina na Qatar kutayarisha madaktari bingwa

Ikiwa ni moja ya sera za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuweka mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya huduma bora za afya kwa watanzania, Dr. Slaa Amekuwa akizunguka nchini marekani ili kujifunza mambo mbali mbali hasa mafanikio ya vyuo kama hivi, na ni jinsi gani anaweza kupata ushirikiano na vyuo hivi ili kutayarisha madaktari wengi wa tiba na mabingwa ili kuiokoa taifa gharama kubwa ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.

Kujibu ombi la Dr. Slaa, rais wa chuo cha tiba, ameahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania chini ya CHADEMA ili kujenga vyuo vya utafiti na tiba nchini Tanzania. Viongozi hao wameweka bayana nia yao ya kuisaidia Tanzania hasa ufisadi na urasimu uliopo utaondolewa. Naye kwa upande wake, Dr. Slaa amemuahidi kwamba, ufisadi utakuwa ni historia katika serikali ya CHADEMA.

Chuo hicho itakuwa tayari kuwatuma madaktari wake bingwa wa kila aina nchini Tanzania kusaidia katika mambo mbali mbali ya tiba itakayoambata na makubaliano na serikali ya CHADEMA ikiwemo kuwafundisha na kuwatayarisha madaktari 4,000 katika kipindi cha miaka (accelerated program
) miwili kama walivyofanya nchini Bangladesh ili kupunguza uhaba wa madaktari. Hawa ni madaktari wasaidizi ambao wanaujuza Fulani. Madaktari wengine watahitaji miaka mitatu ili kuwa madaktari bingwa

0 comments:

Post a Comment