SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 7, 2013

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Atembelea Shirika la Umme la Alabama Power

Katibu Mkuu wa Cahdema Dr Wilbrod Slaa akiwasili Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
Katibu Mkuu wa Cahdema Dr Wilbrod Slaa Akiongozwa na Walinzi muda mfupi baada ya kuwasili Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Akikabidhiwa Kitabu Chenye historia ndefu ya Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akipokea maelekezo Muhimu Kutoka Kwa Uongozi wa Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiongea na Uongozi wa Juu wa Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akipata maelekezo ya kitaalam Kwenye Control Room ya  Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia.Picha Zote na Chadema
----

Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbrod  Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo jana imemfikisha katika kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia

Akielezea baadhi ya shuguli za Alabama Power company, mkurugenzi wa shirika hilo linalojitegemea, ameeleza kwamba shirika hilo linawahudumia wateja million nne tu, huku ikizalisha kiasi cha megawati 48,000 (4.8GW) Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, hakujawahi kutokea mgao wa umeme au umeme kuzimwa hata kwa dakika 5. Panapotokea dharura, kuna kuwepo njia mbadala ya kukabiliana nayo,

Kwa upande wake, Dr. Slaa amejifunza na kugundua kitu kimoja kwamba, watanzania wanaumia kutokana na wachache kuligeuza Tanesco kuwa mradi wao. Dr. Slaa anaamini kwamba mgao tulionao Tanzania, ukosefu wa umeme tulionao ni matunda ya ufisadi wa CCM. Kiongozi huyo anaamini kwamba tatizo ni ccm na desturi yao ya kulindana. ilahali tunatengeneza 600MW huku Waziri Muhongo akidai mwakani tutauza umeme nje ya nchi. Umeme gani wa kuuza nje ya nchi wakati 80% ya watanzania hawana umeme? Huyu mtu yuko katika sayari gani? Miaka 52 ya ufisadi, kugawana vyeo kindugu, umasikini na magonjwa sasa tuseme basi. CCM hawawezi kujidai kwamba watatatua matatizo ya watanzania

Viongozi wakuu Wizarani na Tanesco wanawazuia na kuwadhalilisha wawekezaji kwa manufaa yao binafsi na makampuni yasiyokuwa na huruma na mwananchi wa kawaida. Njia pekee ya kumuokoa mtanzania, ni mtanzania mwenyewe kuamka, na kumng’oa adui CCM kupitia njia ya kura. Mtanzania asifanye kosa tena 2015. Lazima amn’goe CCM ili apate umeme na kuweza kuboresha maisha yake

Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa amejionea jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na mitambo ya kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani yaani, Georgia, Florida, Alabama, Mississini na South Carolina.

Mkurugenzi wa shirika hilo, amemuahidi Dr. Slaa kwamba wako tayari kuja Tanzania na kuisadia nchi hiyo kuboresha uzalishaji, usambazaji pamoja na uendeshaji ikiwa serikali itawahitaji, kwani wameisadia nchi za Philippines na Kuwait ambazo hadi sasa wanazo umeme wa uhakika.

0 comments:

Post a Comment