SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 9, 2013

ZIARA YA MAKAMU WA CCM DK.SHEIN,W​ILAYA MICHEWENI

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na Viongozi wengine alipowasili katika uwanja wa Ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo
katika mkutano wa kuwakabidhi kadi wanachama wapya 50 waliojiunga na Chama hicho katika ziara ya kuimarisha chama Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
 Baadhi ya Wananchi na Wanachama wapya wa Tawi la CCM Kipangani Wete,wakisikiliza Hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa leo alipofanya Mkutano na wanachama hao katika uwanja wa Jamhuri Hall Wete,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kadi mwanachama Mpya wa CCM Khamis Akida Juma,akiwa katika miongoni mwa Wanachama 50 aliowakabidhi kadi leo,akiwa katika ziara ya
                    kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kadi mwanachama Mpya wa CCM Fatma Suleiman Said,akiwa katika miongoni mwa Wanachama 50 aliowakabidhi kadi leo,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)pamoja na Viongozi wa Chama wakila kiapo cha Utii
wakati wa kuwaapisha wanachama wapya waliojiunga na CCM katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,alipofanya zaiara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
 Wanachama Wapya waliojiunga na CCM wakila kiapo cha Utii kwa chama baada ya kukabidhiwa kadi zao na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha
                                   Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba
Mwanachama Mpya aliyejiunga na CCM Amour Suleiman,akijitambulisha kwa wanachama wa CCM Wilaya ya Wete.Jumla ya Wanachama 61 wamejiunga na CCM wakitokea Chama cha CUF,wakati wa Mkutano allioufanya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya hiyo leo,baada ya kuweka jiwe la msingi tawi la CCM Kipangani,
Msanii wa Kizazi Kipya IT, akitowa burudani katika moja ya mkutano wa CCM katika ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM kutembelea Matawi ya CCM Kisiwani Pemba.
NA  ZANZINEWS

0 comments:

Post a Comment