SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 9, 2013

mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare na mwenzake walipofikishwa mahakama kuu jijini dar es salaam jana ambapo walifutiwa mashtaka matatu ya kigaidi kati ya mashtaka manne yaliyokuwa yakiwakabili

Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chama cha demokrasia na maendeleo ChademaWilfred Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Wilfred Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
 Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilfred lwakatare
Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao mbele yake ni mtuhumiwa ludovic
  Ulinzi ndani ya mahakama.
 Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
 Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
wakili wa washtakiwa peter Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
 Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema
 Wilfred Lwakatare akirudishwa rumande
 Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.Picha Zote na Habari na Audiface Jackson
--
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana imemfutia mashitaka mawili ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare.

Jaji aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.

Akizungumza wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa

0 comments:

Post a Comment