SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, April 7, 2013

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka:“Aagiza jengo jengo la ghorofa 16, lililopo Mtaa wa Indira Gandhi katikati ya jijini Dar es Salaam Linalomilikiwa na Ally Raza libomolewe ndani ya siku 30

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
---
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ametoa siku 30 kwa mmiliki wa jengo la ghorofa 16, lililopo Mtaa wa Indira Gandhi katikati ya jiji, Ally Raza kulibomoa jengo hilo baada ya kubainika alilijenga chini ya kiwango.

Kadhalika Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kufanya uchunguzi wa ubora wa majengo mengine matano yanayomilikiwa na Raza ambaye pia ni mmiliki wa jengo lingine la ghoroga 16 lililoporomoka wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kama yako katika viwango vinavyokidhi.

Jengo hilo lililoporomoka lilisababisha vifo vya watu 36, majeruhi 17 na uharibifu wa mali ikiwamo magari linamilikiwa na Raza.

Jengo hilo lilikuwa likijengwa na Kampuni ya Lucky Construction Limited ambayo ni mali ya Diwani wa Kata ya Goba (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Ibrahim Kisoki ambaye pia alijenga jengo jingine jirani na la awali, imetolewa amri ya kufanyika kwa utafiti kubaini kama limekidhi viwango.

Profesa Tibaijuka akizungumza mbele ya Kamati hiyo walipofanya ziara katika jengo hilo jana, alisema uchunguzi wa awali wa kuporomoka kwa jengo hilo umebaini kuwa jengo lililoko mkabala, pia lilijengwa chini ya viwango.

“Ninaagiza jengo hilo kuwa libomolewe ndani ya siku 30 kwa gharama za mmiliki na akikaidi atalipishwa faini ya asilimia mbili ya gharama ya kuendeleza pasipokuwa na kibali kwa kila siku hadi atakapotekeleza agizo hilo,” alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza;

“Makazi haya yanatakiwa kujengwa majengo yasiyozidi ghorofa 10, lakini katika hili ghorofa ambalo linatakiwa kubomolewa kwanza kiutaalamu halikuzingatia vigezo kutokana na kujengwa kwenye kiwanja chenye mita 150 ambacho ni kidogo.”

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembeli alisema kuna taarifa kwamba mmiliki wa jengo anamiliki majengo mengine ambayo hivi sasa yanakaliwa na watu pia yamezua hofu, hivyo yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi.
“Kutokana na majengo yake mawili ambayo tayari yameleta utata kwa kuonekana kujengwa chini ya viwango, hivyo tunataka majengo mengine anayomiliki, Manispaa ya Ilala iyafanyie uchunguzi mapema ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea,” alisema Lembeli.Kwa Habari zaidi BOFYA HAPA 
 

0 comments:

Post a Comment