SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, April 15, 2013

Washindi wa Vodacom MAHELA Waendelea Kujinyakulia MAHELA

Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy(kulia)akifuatilia moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA" inayooneshwa na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(katikati) Mshindi huyo aliejishindia kitita cha shilingi Milioni Tano,ni Bw.Kibwana Kitogo ambae ni mkazi wa Handeni Tanga,anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael. Zaidi ya shilingi Milion 122 bado zinaendelea kushindaniwa,Mteja anatakiwa kutuma neno MAHELA kwenda namba 15544 ili aweze kujishindia fedha taslimu.
Meneja mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akifurahia jambo na bwana. Abdi Mkande (64) Mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam, wakati wa makabidhiano ya fedha alizoshinda kupitia promosheni ya MAHELA, inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Anayeshuhudia na Msaidizi wa Ofisa mkuu wa Biashara - M PESA, wa Vodacom Alice Lushiku.
Msaidizi wa Ofisa Mkuu wa kitengo cha biashara-M-PESA, Alice Lushiku (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa Promosheni ya Mahela Bi. Rose Furahisha, 
( 61 ) mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, aliejishindia shilingi milioni moja kupitia promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. Anayeshuhudia ni Mume wa Bi. Rose bwana, Furahisha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatiliajambo kwa umakini wakati wa kuchezesha Promosheni ya MAHELA inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.

0 comments:

Post a Comment