SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 30, 2013

Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria Watembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Nakukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda

Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  (kulia) akiangalia picha ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria aliyopewa na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano
 Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  (kulia) akimkabidhi picha ya kinyago cha ujamaa Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka nchini Nigeria wako ziara ya mafunzo ya siku tano nchini.
 Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) akimwelezea Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  kuhusu picha ya kinyago kinachoonyesha mtawala wa makabila mbalimbali ya nchi hiyo alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.
Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  (kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
 Kanali Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ)  akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakimsikiliza Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni.
Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja  na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao  kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.Picha na Anna Nkinda-MAELEZO

0 comments:

Post a Comment