SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 10, 2013

Tigo Ngorongoro Run yafana.

Washiriki wakijiandaa tayari kwa ajili ya kuanza mashindano wakiwa pamoja na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu pamoja na waandaaji Kampuni ya Zara Tours na kudhaminiwa na Kampuni ya TIGO.
washiriki wakitimua vumbi.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akimtoka  Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio za mapambano dhidi ya Malaria yenye lengo la la kuwaelimisha wananchi namna ya kupambana na malaria , ugonjwa ambao unapoteza  mamilioni ya Watanzania kila mwaka,  zilizoandaliwa na Kampuni ya Zara Tours na kudhaminiwa na Kampuni ya TIGO katika mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa wa Mbio za mapambano dhidi ya Malaria Bwana Dicksoni Marwa.
Mwimbaji  wa  bongo fleva Barnaba Elias (Barnaba boy) akiwa na Irene Kiwia mkurugenzi  kutoka kampuni ya Frontline Porter Novelli  ambao walimaliza mbio hizo hadi  mwisho.
Mshiriki mwenye umri  mkubwa kuliko wote mzee Jarome mollel(70) ambaye alimaliza mbio za kilometa tano(5).
NA DEWJI BLOG

0 comments:

Post a Comment