Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Bwana Frans Timmermans jijini The Hague Uholanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Malkia Beatrix wa Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake Rasmi jijini The Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi kwa Ziara rasmi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya mboga ya Rijk Zwaan Bwana Kees Reinink akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya miche inayotokana na mbegu bora wakati Rais alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague,nchini Uholanzi jana. Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Bwana Geoffrey Kirenga.Kampuni ya RIJK ZWAAN tayari imewekeza nchini Tanzania huko Arusha ambapo inazalisha mbegu bora za mazo ya mbogamboga zilizofanyiwa utafiti kudhibiti magonjwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.
(Picha na IKULU)
0 comments:
Post a Comment