ZANZIBARI SINGER BI KIDUDE DIES
Tanzanian singer Fatma binti Baraka, known as Bi Kidude, has died at her home on the island of Zanzibar.
Thought to be more than 100 years old, she was a legendary performer of Taarab, a style of Swahili Arab-influenced music.
In 2005, she was awarded a prize for her contribution to world music at Womex, the annual gathering of the world music industry.
She continued performing and touring until recently.
Correspondents say Bi Kidude's performances were known for their intense energy; she often beat a large drum and danced on stage as she sang.
She also broke Muslim taboos by openly smoking and drinking alcohol, they say.According to Womex, she started her career as a Taraab singer in the 1920s.
"She not only helped to maintain the cultural heritage, but also reinvented it, infusing it with local rhythms, Swahili language and matters of everyday life," Womex said about her in 2005.
The singer's exact date of birth is not known, but she is believed to have been born in 1910.
Bi Kidude was the subject of a documentary, As Old as My Tongue, a few years ago which reported that she began breaking rules at an early age, running away from a Koranic school at the age of 10.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) katika sherehe za kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam mapema mwaka huu,(katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi. Baadhi ya wengine waliotunukiwa nishani hizo za masuala mbalimbali ni pamoja na Jaji mstaafu Eusebia Munuo, Balozi Ombemi Sefue, Reginald Mengi na wengineo.
Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar.
Gari ikiwa na Mwili wa marehemu Bi Kidude ukiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi kesho mchana na kuzikwa Kitumba. Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Ndugu na Jamaa wakiubeba mwili wa marehemu BiKidude wakati ulipowasili nyumbani kwake Rahaleo kwa ajili ya maziko kesho.
SALAMU ZA RAIS KIKWETE KWA MSIBA WA BI KIDUDE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia taarifa za kifo cha Msanii Mkongwe hapa nchini, Marehemu Fatma Binti Baraka Hamisi ambaye alijulikana sana kwa jina la kisanii la Bi. Kidude aliyefariki dunia tarehe 17 Aprili, 2013 akiwa nyumbani kwake katika eneo la Bububu, Zanzibar kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia taarifa za kifo cha Msanii Mkongwe hapa nchini, Marehemu Fatma Binti Baraka Hamisi ambaye alijulikana sana kwa jina la kisanii la Bi. Kidude aliyefariki dunia tarehe 17 Aprili, 2013 akiwa nyumbani kwake katika eneo la Bububu, Zanzibar kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Msanii Mkongwe na Mwimbaji Mashuhuri wa Nyimbo za Mwambao hapa nchini, Marehemu Fatma Binti Baraka Hamisi maarufu kwa jina la Bi Kidude aliyefariki tarehe 17 Aprili, 2013 akiwa nyumbani kwake eneo la Bububu, Zanzibar kutokana na ugonjwa wa Kisukari”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema alimfahamu Bibi Fatma Binti Baraka enzi za uhai wake kutokana na mchango wake mkubwa ndani na nje ya nchi yetu katika nyanja za Sanaa na Utamaduni ambapo alimudu kuitangaza vyema nchi yetu kupitia kipaji chake cha uimbaji kwenye matamasha mbalimbali aliyowahi kuhudhuria na uimbaji wake kuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi waliowahi kuhudhuria matamasha hayo, kuyasikiliza kwenye Radio na kuyatazama kupitia matangazo ya Televisheni.
“Kwa hakika Fani ya Sanaa na Utamaduni imempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika sana katika kuinua zaidi kiwango cha uimbaji wa Muziki wa Mwambao ambao umejizolea sifa nyingi”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake na kuongeza,
“Kufuatia taarifa hizo za kusikitisha, ninakutumia wewe Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa Wasanii nguli wa Muziki wa Mwambao hapa nchini”.
“Vilevile naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa Wanafamilia, ndugu na jamaa wa Marehemu Bibi Fatma Baraka Hamisi kwa kupotelewa na mhimili madhubuti wa familia. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu. Amina”, amesema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete amewapa pole Wasanii wote hapa nchini ambao kwa hakika watakuwa wameguswa sana na kifo cha Bibi Fatma Baraka ambaye alichangia vilivyo katika kuitangaza sanaa kupitia uimbaji wa Muziki wa Mwambao. Amesema “kwa wao, njia bora ya kumuenzi Bi. Kidude ni kuendeleza zaidi sanaa ya uimbaji wa Muziki wa Mwambao na kuyaenzi yote mema na mazuri aliyolifanyia Taifa letu.”
Rais Kikwete amewahakikishia wanafamilia, ndugu na jamaa wa Marehemu Fatma Baraka kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
17 Aprili, 2013
*****
Nguli wa Muziki wa Mwambao nchini na barani Afrika Fatuma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude (zaidi ya miaka 90) amefariki mchana huu.
Taarifa zilizoifikia zinasema kuwa Bi Kidede amefariki majira ya saa 7 mchana wa leo nyumbani kwa ndugu yake huku Bububu Kisiwani Zanzibar.
Aidha taarifa hizo zinaelezo kuwa Mipango yua kuusafirisha mwili wa Marehemu inafanyika kutoka huko Bububu hadi Nyumbani kwake Raha Leo.
Bi Kidude aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa na kulazwa mara kadhaa kifo chake kinaelezwa pia kuchangiwa zaidi na umri mkubwa.
Msiba huu ni mzto kuwahi kutokea kwa tasnia ya muziki na Sanaa kwa ujumla kufuatia Mchango mkubwa wa Marehemu katika kukuza muziki halisia wa mwambao.
Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Bi Kidude Nishani ya Uhuru wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi cha uhai wake.
--
WASIFU WA MAREHEMU FATUMA BINTI BARAKA 'BI KIDUDE'
Marehemu Bi Kidude alikuwa ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika. Jina lake halisi ni Fatuma binti Baraka. Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu.
Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrikaumekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
Leo hii ni Marehemu! Nguli na Mtunukiwa wa Nishani ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania 2012, Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar.
Bi Kidude aliwahi kusimulia kuwa hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
Bi Kidude aliendelea kusema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.
Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.
Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya 'wanja' na 'hina' ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa 'Unyago' na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.
Watu wanasema 'Utu uzima dawa' Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar.
Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.
Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake.
Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa Jang'ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.
Bi Kidude pia amekuwa akishirikishwa na wasanii wengi wakongwe na chipukizi katika nyimbo zao. Miongoni mwa nyimbo zinazotamba sana siku hizi ambazo Bi Kifude ameimba na vijana wa kisasa ni za Msanii Ali Toll maarufu AT.
Mbali na AT lakini pia Bi Kidude amewika na kung'ara zaidi katika wimbo mwingine wa vijana wa Ahmada Umelewa wa Msanii Offside Trick ambao umepigwa marufuku kupigwa kwa sasa visiwani Zanzibar.
R.I.P FATUMA BARAKA “BI KIDUDE”.
CREDIT TO H@KI NGOWI
Simanzi Yatawala Msiba Wa Bi. Kidude Zanzibar Leo
CREDIT TO H@KI NGOWI
Simanzi Yatawala Msiba Wa Bi. Kidude Zanzibar Leo
MRAJIS wa Baraza la Sanaa Zanzibar (BASAZA), Khadija Batash akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
MTENDAJI wa Busara Promotions, Stela Steven akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbali mbali wakiwa kazini katika makaazi ya Msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki kwa msanii huyo.
WATENDAJI wa Busara Promotins wakijadiliana jambo nje ya nyumba ya msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki.
MJUKUU wa marehemu Bi Kidude, Bwana Baraka, akitoa taarifa za mazishi kwa waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Rahaleo mjini Zanzibar.
WAFIWA wakiwa nyumbani kwa marehemu.
MKURUGENZI wa Kikundi cha Taarab cha TAUSI, Mariam Hamdani akizungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwa marehemu Bi Kidude.
Sihaba Ismail mmoja wa watu waliofundishwa kazi za kufunda wari na dawa asilia na Bi Kidude akielezea anavyomfahamu marehemu.
MSANII wa Taarabu asilia, Makame Faki akielezea jinsi Bi Kidude alivyokua akiimudu sanaaa ya taarabu na unyago.
Picha zote na Haroub Hussein wa Globu ya Jamii, Unguja
0 comments:
Post a Comment