SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 17, 2013

MGIMWA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MIKUTANO YA KIPUPWE MJINI WASHINGTON DC MAPEMA WIKI HII.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt  William Mgimwa Kulia.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda pamoja na Kamishna wa Sera Bw. Beda Shallanda.
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor  pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul Mwafongo.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya Fedha Bw. Patric Pima.
Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC
****
MIKUTANO ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Augustiao William Mgimwa ni Gavana mmoja wapo katika mikutano hiyo na Nchi ya Tanzania ni mwanachama katika mikutano hii.

Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. 

Aidha pamoja na mikutano hiyo kunakuwa na semina na majadiliano mbalimbali, mikutano ya waandishi wa habari na matukio mbalimbali yanayohusu uchumi jumla , maendeleo ya kimataifa na masoko ya kifedha ya kimataifa.

Mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Magavana wa Benki itakuwa kipindi kijacho baada ya mikutano hii.

Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia  na Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa  kwa kawaida wanakutana mara moja kwa mwaka  kujadili kazi zinazohusu taasisi  zao. Mikutano ya mwaka ,  inayofanyika mwezi Septemba  / Oktoba huwa inafanyika  mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na mwaka wa tatu huwa inafanyika kwa nchi  mwanachama.

Uzinduzi wa Mikutano hii ya Bodi ya Magavana ilifanyika Sanannah, Georgia, USA mwezi March mwaka 1946. Mkutano wa kwanza wa mwaka ulifanyika mjini Washington DC mwaka 1946.


Katika mikutano hiyo ya mwaka makundi  ambayo ni  kamati za fedha, kamati za  maendeleo, Nchi za kundi la kumi,  Nchi za kundi la ishirini na nne na makundi mbalimbali ya nchi wanachama wanafanya  majumuisho ya mikutano hiyo na  kila kundi linawasilisha makubaliano yao katika mkutano mkuu wa mwaka.

 Mikutano ya mwaka inakuwa na utangulizi wa mkutano wa siku moja ambapo Bodi ya Magavana wanafanya maamuzi ya namna mambo ya sasa ya Shirika la Fedha la Kimataifa yanatambulika na kupitisha maazimio husika. 

Katika Mikutano hiyo ya mwaka, mwenyekiti wake anakuwa Gavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, na uenyekiti huo ni wa  mzunguko kati ya nchi wanachama kila mwaka. Kila baada ya miaka miwili wanachagua Wakurugenzi watendaji. Kila mwaka wanakaribisha wanachama wapya kuingia katika shirika la fedha la kimataifa na Benki ya Dunia.


Kwakuwa mikutano ya mwaka inakusanya namba kubwa ya nchi wanachama wanaotambulika rasmi  kwa pamoja, wanatoa nafasi ya ushauri  mkubwa na mdogo, uliorasmi na usio rasmi. Semina mbalimbali zinafanyika sanjari na mikutano hiyo, ikiwahusisha waendesha semina kwa wanachama ambao ni wafanyakazi na waandishi wa habari.  Mikutano ya mwaka imeweka semina ambazo zitalenga katika makongamano ambayo yanajenga na yanahusisha sekta binafsi, wawakilishi kutoka serikalini na maofisa wakuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa na wafanyakazi wa Benki ya Dunia. Somo la fedha  za kimataifa  ambalo kila mwaka linatolewa kwa na  Per Jacobsson  kwa ufadhili wa  Taasisi  iliyoanzishwa kwa heshima ya  Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa,  pia inatolewa kila mwaka sambamba na mikutano hiyo.

Mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia iliyofanyika nje ya Washington DC  kuanzia mwaka 1947—2012
Mwaka
Mahali
1947
London
1950
Paris
1952
Mexico City
1955
Istanbul
1958
New Delhi
1961
Vienna
1964
Tokyo
1967
Rio de Janeiro
1970
Copenhagen
1973
Nairobi
1976
Manila
1979
Belgrade
1982
Toronto
1985
Seoul
1988
Berlin
1991
Bangkok
1994
Madrid
1997
Hong Kong
2000
Prague
2003
Dubai
2006
Singapore
2009
Istanbul
2012
Tokyo

Mikutano hii itaendelea hadi mwishoni mwa wiki ijayo na washiriki wengi wanazidi kuingia mjini hapa.
Imetolewa Na Msemaji Mkuu 
Wizara Ya Fedha 
Bi Ingiahedi Mduma 
Washington DC
 16/04/2013

0 comments:

Post a Comment