SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, March 21, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI DARAJA LA SUKA - GOLANI KIMARA JIJINI DAR


  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo-Chadema, John Mnyika.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik, Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kulia ni Mbunge wa Ubungo-Chadema Mhe. John Mnyika.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo-Chadema, John Mnyika wakati alipokwenda kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuf Mwenda na Mbunge wa Ubungo-Chadema John Mnyika.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waishio eneo la Golani  Kimara Suka muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani.
 Wananchi wa vyama mbalimbali vya Siasa wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana mchana.
(Picha na Freddy Maro-IKULU)

0 comments:

Post a Comment