Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwana Sunil Colaso, akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Yatosha inayomwezesha mteja wa Airtel kupata dakika za muda wa maongezi, sms na ushi cha internet.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya, akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi, sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa simu kadi moja, taifa moja, bei moja.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando, akielezea huduma mpya ya Airtel Yatosha yaani simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayomwezesha mteja wa Airtel kuwasiliana na mitandao yoyote nchi na kupata kifurushi cha muda wa maongezi, sms, na internet kwa bei nafuu hadi shilingi 349/= pichani (katikati) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya akifuatiwa na Meneja Masoko Airtel, Anethy Muga.
AIRTEL YAZINDUA GHARAMA NAFUU ZAKUPIGA SIMU MITANDAO MINGINE
* Airtel yadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja - Wateja nchini kufaidika na kiwango cha chini cha hadi 75% kupiga simu popote bila kikomo* Piga simu muda wowote usiku na mchana.
Dar es Salaam Jumatano Machi 20, 2012: Airtel Tanzania leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama "AIRTEL YATOSHA" itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu cha hadi asilimia 75 bila kuwa na sababu kubadili laini kwa kuhofia gharama.Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakachowapa muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja.Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso alisema " Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila Mtanzania, hii itawarahisishia Watanzania wote kupata mawasiliano nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini. Kupitia kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba mteja atapata dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS 100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha internet cha 25MB ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku.
Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndiyo sababu kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi nzima thamani ya pesa zao.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya alisema "Airtel YATOSHA ni huduma inayopatikana kwa SIKU au kwa WIKI hivyo mteja anapewa nafasi ya kuchagua anachokata. Katika mpango wa WIKI mteja atatozwa shilingi 1,999 na kupata dakika 70, sms 700 na kifurushi cha internet cha 175MB.
Kujiunga na huduma hii mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kuunganishwa moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchangua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet. Dakika za maongezi zitatumika kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa saa 24 na gharama za kupiga simu zitatozwa kwa sekunde.
Kuhusu muda wa kujiunga na Airtel YATOSHA mteja anaweza kujiunga wakati wowote kati ya saa 11:00 asubuhi hadi 5: 59 usiku.
Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zenye ubora na ubunifu nchini. Na hii ni njia nyingine ya kudhihirisha jinsi Airtel inavyotoa huduma za mawasiliano yenye ubora na gharama za ushindani kwa Watanzania. Airtel itaendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa kutoa huduma bora zenye gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment