SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 30, 2013

Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal Afika na Kujionea Jengo la Ghorofa ya 15 Kuanguka Jijini Dar es Salaam


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghandi na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe jana asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
 Uokoaji ukiendelea.....
Askari Jeshi wakikokota Jenereta kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha mwanga unapatikana kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya giza kuingia.
Picha na Muhidini Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais.

0 comments:

Post a Comment