Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara wa Mtwara kuhusu
mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2013.
---
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi
wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi watakavyonufaika na gesi
itakayozalishwa mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es
Salaam.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia
amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka
jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga
mpango wa kusafirisha gesi hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho
uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku
mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi
itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi
ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki
yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote
ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu…
kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka
Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia
viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema
Pinda na kuongeza:Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.........>>>
0 comments:
Post a Comment