Meza kuu katika mkutano wa umoja wa Watanzania Ujerumani.
Watanzaia waishio Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja wao.
Watanzania waishio nchini Ujerumani wakijiachia kwa mduara.
Mhe. Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU.
Kamanda Ras Makunja wa FFU (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi.
Huyu binti mdogo naye alikuwepo.
Umoja Wa Watanzania Ujerumani Wapata Uongozi Mpya
Mkutano mkuu wa Watanzania waishio Ujerumani uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake mojawapo ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo. Kabla ya kufanyika uchaguzi huo na mjadala wa maazimio ya umoja huo, Mgeni rasmi katika mkutano huo mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani,Mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwa Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo.
Kwanza aliwapongeza Watanzania kwa kufanikiwa kuunda umoja huo wa Watanzania waishio Ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa Watanzania wote nchini
Ujerumani. Bw. Ali Siwa aliwaambia Watanzania kwamba ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri wowote utakaoleta maendeleo ya umoja huo na Watanzania kwa ujumla aliwaasa Watanzania kuwa na mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa ufunguo na sauti ya maendeleo yao na vizazi vyao ugenini na nyumbani pia.
Baada ya nasaha hizo wananchama wa umoja wa Watanzania walichagua viongozi wao kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti: Mfundo Peter Mfundo.
Makamu Mwenyekiti: George Mtalemwa.
Katibu: Bi Tulalumba Mloge.
Mweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.
Umoja huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili kwenye serikali ya Ujerumani na kutambuliwa kisheria ambacho kinawaunganisha Watanzania wote wanaoishi Ujerumani na ndio Daraja linalowaunganisha Watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni.
Kwa Watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) milango ipo wazi, wasiliana na kamati.utu@googlemail.com
0 comments:
Post a Comment