Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, kimefungua daftari la watu wanaotaka kuania uongozi wa chama, ambao utaaniwa tena mwezi Disemba.
Rais Jacob Zuma anatarajiwa kupingwa na naibu wake, Kgalema Motlanthe kuania urais.
Wanachama milioni 1.2 wa ANC watachagua nani wa kumuunga mkono.
Katika miaka ya karibuni watu wa kabila la Zulu, kabila la Rais Zuma, wameingia kwa wingi zaidi kwenye chama; lakini wadadisi wanasema rais Zuma atapata shida kushikilia wadhifa wake.
Uchumi wa Afrika Kusini umezorota, na mauaji ya wachimba migodi yaliyofanywa na polisi yamepunguza hadhi ya Rais Zuma.
Habari Na BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment