Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Freight Forwarders Ltd, Chris Lukosi (kushoto) akikabidi misaada kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiq.
Chris Lukosi (katikati) na Mecky Sadiq, wakisalimiana kabla ya makabidhiano.
Wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengine baada ya makabidhiano.
KAMPUNI ya kusafirisha mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd) yenye makao yake jijini Londo, Uingereza, leo imekabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiq, mizigo ya misaada kwa ajili ya watu ambao sasa wanaoishi Mabwepande baada ya kuhamia huko kutoka sehemu za mabondeni jijini Dar es Salaam kutokana na mafuriko yaliyozikumba sehemu hizo mwanzoni mwa mwaka huu.
Akikabidhi misaada hiyo ambayo imechangwa na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza, kiongozi wa kampuni hiyo, Chris Lukosi, alisema katika kuhakikisha misaada hiyo haina matatizo kuwafikia wahusika, kampuni hiyo iliisafirisha bure na kuilipia ushuru.
Lukosi aliwashukuru wote waliochangia ikiwa ni pamoja na Mtanzania, Jestina George na taasisi ya Urban Pulse ya Uingereza kwa kushiriki katika kukamilisha zoezi hilo.
Akipokea misaada hiyo kwa wakazi wa Mabwepande, Mecky Sadiq, aliipongeza hatua hiyo na kuwataka watu wengine kuiga mfano huo wa kuwasaidia watu walio na matatizo.
0 comments:
Post a Comment