SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, August 10, 2012

TAFF YATOA TAMKO KUPAMBANA NA MAHARAMIA WA FILAMU

Mwenyekiti wa Bongo Muvi , Jacob Steven ‘JB’ (kushoto)  akizungumzia vita dhidi ya uharamia wa filamu uliofanywa na Kampuni ya Steps Entertainment  kwa kushirikiana na wasanii kadhaa.  Kulia ni msanii wa filamu, Vincent Kigosi 'Ray' na katikati ni Mwenyekiti wa TAFF,  Simon Mwakifwamba.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (katikati) akizungumzia  uamuzi  dhidi ya wizi wa sanaa za wasanii.  Kushoto ni msanii, Mahsein  Awadhi  (Dk. Cheni) na kulia ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi ,Jacob Steven  'JB' . Msanii wa filamu nchini, Mohamed Nice 'Mtunisi' (kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.  Kushoto kwake ni Dk. Cheni na Msama.
SHIRIKISHO la Filamu nchini (TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  na  kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana,  viongozi wa umoja huo kwa pamoja walisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo imekuwa ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao,” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongo  Muvi,  Jacobo Steven ‘JB’,  alisema serikali inapaswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua  kufanya kazi zao kwa nguvu zote.
Kwa upande wake Meneja wa Usimamizi kutoka TRA, Msafiri Ndimbo,  alisema mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari mwakani hasa baada ya serikali, kupitia bunge, kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
                                             Picha na:   www.burudan.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment