SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, August 10, 2012

LOBAL PUBLISHERS YAZINDUA SHINDANO LA ‘SHINDA NOAH’

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugence Isakefu, Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota na Mratibu wa shughuli mbalimbali za Glabal, Juma Mbizo.
Isakefu (katikati) akizungumza katika hafla hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) akiipongeza Global Publishers kwa hatua yake hiyo ya “kuwakumbuka” wasomaji na wananchi kwa jumla. Kushoto ni Abdallah Mrisho na kulia ni Richard Manyota.
Abdallah Mrisho akionyesha mojawapo ya simu aina ya Samsung Galaxy ambazo zitashindaniwa sambamba na Noah hiyo.Kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally na kulia ni Flugence Isakefu.
Isakefu akifungua mlango wa gari aina ya Noah linaloshindaniwa.
...Akizindua shindano hilo.
Gari aina ya Noah linaloshindaniwa.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo..PICHA: ERICK EVARIST NA RICHARD BUKOS / GPL
---
KAMPUNI ya Global Publishers ambayo huchapisha magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, leo imezindua rasmi shindano la ‘Shinda Noah’ katika ofisi zake zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo wa uzinduzi, Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho, amesema huo ni utaratibu ambao kampuni imejiwekea kurudisha sehemu ya mapato kwa wateja wake na kama ilivyokuwa kwa miaka mitano iliyopita, mwaka huu gari aina ya Noah litatolewa.


“Mbali na zawadi hiyo ya gari, zawadi nyingine ambazo ni simu za mkononi, televisheni, na nyingine kibao zitatolewa kwa wasomaji wa magazeti pendwa na kwa kutuma kuponi kwa anuani elekezi,” alisema Mrisho.


Mgeni rasmi katika promosheni hiyo inayoanza mwezi huu wa Agosti na ambayo itafikia kikomo mwezi Novemba, alikuwa ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugence Isakefu, ambaye alifika kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana.

0 comments:

Post a Comment