Ni Ofa mpya ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet kwa shilingi 250 tu kwa siku.
· Ofa kuanza kila siku saa tano usiku hadi saa moja asubuhi.
· Kupata ofa hiyo piga *102*250#
-
Dar es Salaam 25th Julai 2012….
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imeanzisha ofya mpya ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo itawawezesha wateja wa mtandao huo kupiga simu bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kupata huduma za intanet kwa shilingi 250/= tu kwa siku.
Ofa hiyo mpya itakuwa ni kwa siku saba za wiki kuanzia saa tano usiku hadi saa moja asubuhi katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ili mteja ajiunge na huduma hiyo, atatakiwa kupiga *102*250# ambapo ataweza kupiga simu kutoka Vodacom kwenda Vodacom, kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda mitandao yote ya simu na kutumia intanet bila kikomo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meza alisema kipindi hiki ni maalum kwa waislamu duniani kote kuwa karibu na Mungu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
“Tumeona vyema tuwapatie njia rahisi ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa unafuu na ambayo wataifurahia tukijua kwamba waislamu walio wengi ni miongoni mwa wateja ambao wametuunga mkono kwa miaka mingi sasa. Tunataka nao wajisikie kuwa sehemu ya familia ya Vodacom katika kipindi hiki cha maombi,” alisema Meza.
Ofa hii imekuja wakati Vodacom Foundation inaendelea na kampeni yake ya Care and Share mkoani Tanga inayolenga kutoa misaada ya kifedha na vifaa mbalimbali kwa watoto yatima katika kipindi cha Mwezi wa Ramadhan.
Kampeni ya Care and Share inaadhimisha miaka mitano tangu kuzinduliwa kwake, huku ikitoa fursa ya kipekee kwa Vodacom Foundation kushughulikia changamoto mbalimbali kwa watoto yatima na vituo vya kulelea watoto yatima.
Kupitia kampeni hiyo, mamia ya watoto yatima wameweza kusaidiwa na maisha yao kuboreshwa, suala ambalo jamii nzima na wateja wa Vodacom wanajivunia.
“Tutaendelea kuwapatia wateja wetu kile wanachostahili kwani bila ya mchango wao Vodacom Tanzania isingekuwa hapa ilipo leo. Nawatakia waislamu wote kheri katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan,” alihitimisha Meza.
Mwisho……
0 comments:
Post a Comment