MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Iddy
MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewata wakazi jijini hapa kutambua kuwa watendaji wanaosema anashindwa kumwajibisha mkurugenzi wa jiji Juma Iddy kwakuwa na ndugu yake ni wapotoshaji.
Kandoro aliyasema hayo ktika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilicholenga kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watendaji wanaozusha undugu kati yake na mkurugenzi wakati hata kwao hakufahamu.
Alisema watendaji hao wamefikia hatua ya kumuandikia barua wakimtaka amwajibishe licha ya kuwa ni ndugu yake wakidai utendajikazi wake una kasoro nyingi.
Alisema kwa uchunguzi alioufanya ametambua kuwa watendaji hao ni wale ambao awali waliigeuza halmashaueri hiyo kama shamba la bibi na kuiba kwa kadiri walivyoweza lakini hivi sasa mianya hiyo imezibwa.
Alisema kutokana na kukosa nafasi ya kuiba ndiyo maana wanamchukia mkurugenzi huyo kwakuwa wanaamini tangu afike wameshindwa kuendelea na tabia yao mbayo ya kutafuna bila aibu fedha za serikali.
Alisema yawezekana kweli mkurugenzi huyo akawa na mapungufu yake lakini serikali ina nufaika kwa kiasi kikubwa kwa uwepo wa mkurugenzi huyo kutokana na ukali wake kwenye kutetea fedha za umma.
Alimtaka mkurugenzi huyo kuendelea na kasi hiyo akisema serikali inahitaji watu wa namna hiyo wanaochukiwa na wezi kwakuwa wanadhibiti mianya inayoweza kutumiwa na wachache kujinufaisdha kwa fedha za maendeleo ya walalahoi.
0 comments:
Post a Comment