SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 27, 2012

Bahanuzi: Nataka kwenda Sauz


Said Bahanuzi.
Na Lucy Mgina
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amesema anatamani kujiunga na moja ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa kuwa anaamini ni bora zaidi katika Bara la Afrika.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bahanuzi alisema malengo yake yatatimia siku akifanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaocheza katika ligi hiyo kutokana na kuamini ni bora zaidi.
Alisema wachezaji wanaocheza katika ligi hiyo wanajituma kwa nguvu hali inayosababisha kuwe na ushindani mkubwa kwa timu zote. “Katika maisha yangu ningependa zaidi kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini kutokana na ligi yao kuwa imara na ya ushindani mkubwa ukilinganisha na nchi zingine hapa barani Afrika.
“Ukiangalia wenzetu huko wanacheza kwa nguvu zaidi na ligi yao imekuwa katika kiwango cha juu zaidi, hasa kwa wachezaji na masuala ya udhamini,” alisema Bahanuzi aliyetua Yanga akitokea Mtibwa Sugar, ameonyesha uwezo mkubwa katika michuano ya Kagame.
NA GPL

0 comments:

Post a Comment