SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, April 22, 2012

ZUWENA KIBENA ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA NGUMI YA TAIFA NA KUTOA AHADI



Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena ' Mama Kanali Kipingu'  akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliyopo Kibaha, Mkuza mkoa wa Pwani jana na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hao.


Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena ' Mama Kanali Kipingu' akikabidhi pesa ya maji kwa nahodha wa timu ya Taifa ya Masumbwi Seleman Kidunda.

Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena ' Mama Kanali Kipingu' akiwa katika picha ya pamoja na mabondia hao jana.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
---
MWAKILISHI wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena 'Mama Kanali Kipingu' jana alitembelea kambi ya timu ya ngumi ya Taifa na kuwaasa wawe makini wanapokwenda kwenye michuano ya kufuzu mashindano ya Olimpiki.
Akizungumza na mabondia hao kambini kwao Kibaha, Mkuza mkoa wa Pwani, 'Mama Kanali Kipingu' alisema licha ya kwamba kambi ilikuwa na ugumu wa aina fulani lakini wahakikishe wanarudi na medali kwa watu wote watakaokwenda katika mashindano hayo.
Alisema anajua mabondia wote wapo katika hali nzuri na pia nafasi za kufuzu michuano hiyo ni chache hivyo wanatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii kwani siku zilizobaki ni chache.
"Nimeamua kuja kuwatembelea ili kuwapa hamasa na mjue kama tupo nyuma yenu, lakini sitaondoka bure ninawapa hii sh. 50,000/= kwa ajili ya kununulia maji na vitu vingine vidogo vidogo na kwamba bondia atakayerudia na medali ataandaliwa zawadi maalum na BFT," alisema 'Mama Kanali Kipingu'.
Aliongeza kuwa, kesho Jumatatu watakuwa na kikao ambacho kitajadili ni zawadi gani watakayotoa kwa bondia atakayerudi na medali na pia aliahidi kuisaidia BFT kulipa deni wanalodaiwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (AIBA).
Katika hatua nyingine, Zuwena ambaye anaupenda sana mchezo huo, alisema yupo mbioni kutoa tuzo kwa makocha ambao walifanya vizuri katika miaka iliyopita lakini bado mpaka hivi sasa wanauendeleza mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment