SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, February 27, 2012

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda Apokea Msaada wa Vifaa vya Kutolea Huduma za Afya



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kutolea huduma za afya zikiwemo dawa za kutibu ugonjwa wa kichocho na maabara ndogo za kubaini dawa zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ujerumani ya MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali Dkt.Karl-Ludwig Kley leo jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali nchini na vituo vya afya vilivyo mipakani
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(katikati) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuja wakifuatilia maelezo ya kitabu cha mwongozo wa maabara ndogo inayohamishika ya kubaini dawa zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) yaliyokuwa yakitolewa na balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda juu ya dawa zilizotolewa leo jijini Dar es salaam na kampuni ya Ujerumani ya MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuji.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

0 comments:

Post a Comment