SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 25, 2012

SUPER D BOXING COACH AWANG'ARISHA MAKOCHA WENZIE BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO YA KIMATAIFA

Mkufunzi Mkuu wa Makocha wa Ngumi kutoka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani ( AIBA), Josephe Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa, Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani, katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini, Makore Mashaga na kushoto ni Kocha wa Timu ya Polisi Mohamed Hashimu.
Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani jana huku wakiwa wameng'arishwa na fulana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao.
Baadhi ya Makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika pozi baada ya kuhitimu mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyokuwa yakifanyika Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani.
Picha  na SUPER D

0 comments:

Post a Comment