SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, December 9, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL ALIPOSHIRIKI MKESHA WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Leo ni miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hata hivyo, shamra shamra za kufikia kilele zilianza muda na jana kulikuwa na mkesha nchi nzima ulioandamana na mapambo ya kila namna. Hapa ni eneo maarufu la Mnara wa Askari jijini Dar es Salaam likimeremeta jana usiku na kubadilisha mandhari yake yaliyozoeleka ikiwa ni sehemu ya kukaribisha siku hii muhimu ya leo.
 Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 8 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck sadick, akizungumza jukwaani kutoa salam za sherehe hizo kwa wananchi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyesha Rimoti  kufyatua Mafataki ikiwa ni sehemu ya kuzindua rasmi Mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kutoka (kushoto) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Koba, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria Mkesha wa Sherehe za Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru.
 Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.
 Kapten John Komba, akiongoza kundi lake la Kwaya kuimba wimbo maalum wa Maadhimisho ya Sherehe hizo jukwaani.
 Baadhi ya Wabunge na wananchi wakimtunza Kaptein John Komba wakati akiimba jukwaani.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
 Wanenguaji wa Bendi ya TOT Plus, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
 Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani maalum ya kusherehekea sherehi hizo.
 Mbunge John Shibuda, akipagawishwa na ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo, iliyokuwa ikipigwa na wasanii wa kundi  la JKT Mgulani.
 Wasanii wa kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakimpagawisha Mbunge Msindai, jukwaani  wakati wakishambulia jukwaa.
 Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kupitia Chama cha Wananchi CUF, Hamad Rashid, akijumuika na vijana wa CCM pamoja na Msindai kucheza miondoko ya Taarab, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Kundi la Sanaa la Safi Theatre wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma na Sarakasi mbele ya jukwaa Kuu.
 Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
 Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
 Vijana wakishangia burudani iliyokuwa ikitolewa jukwaani na makundi mbalimbali ya sanaa, wakati wa sherehe hizo. 
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais.

0 comments:

Post a Comment