SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, July 4, 2011

Taswira Za Wadau Wa Shinyanga Walivyopagawishwa na Msimu wa Dhahabu wa Serengeti Fiesta 2011


Msanii wa kizazi kipya anaekuja juu kwa sasa aitwaye Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani mbele ya mashabiki wa tamasha la msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti fiesta 2011 jioni ya Jana kwenye uwanja wa Kambarage,ambapo wakazi wa Shinyanga walijitokeza kwa wingi.
Kicha mahiri katika miondoko ya Hip hop Bongo,Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua jukwaani jioni ya jana kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2011.Tamasha la Serengeti Fiesta linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd ikishirikiana na Clouds Media Group,wakati huo huo mdhamini mkubwa wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd kupitia kinywaji chake maridhawa kabisa,Serengeti Primeum Lager.
Mkali mwingine wa hip hop Bongo akitokea jijini Arusha,JCB akiwaangushia madini wakazi wa shinyanga jioni ya jana
 Baba Jonii  Adam Mchomvu nae alikuwepo kuwiambisha wakazi wa Shinyanga
Mzee wa Robo saa a.k.a Amin kutoka THT akitumbuiza jukwaani na baadhi ya nyimbo zake ikiwemo ya robo saa,bora nikimbie pamoja singo yake mpya iitwayo Mapenzi yameteka Dunia.
Msanii mahiri wa kizazi kizazi kipya,Mwasiti akiimba pamoja na shabiki wake jukwaani jioni ya jana ndani ya uwanja wa kambarage wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2011 likiendelea.
Mheshimiwa Themba akicheza na shabiki ambaye aliomba apande jukwaani nae ajiachie pamoja na ulemavu wake.
 Baadhi ya wasanii wa mkoani Shinyanga wakiwa jukwaani mchana huu tayari kwa amsha amsha kwa tamasha la Serengeti Fiesta 2011 ndani ya uwanja wa Kambarage,
Kutoka Kiumeni,Wasanii mahiri wa bongofleva Chege na Themba pichani juu na chini wakiwaimbisha wakazi wa Shinyanga kwa namna ya kipekee kabisa jioni ya jana kwenye tamasha la Serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Kambarage,ilikuwa ni full kushangweka bila Majotro kabisa.
Aahhhhhh mbona kwa sana tuu....kitu cha Golden moment kipo hapa.
Shinyanga nayo aaaahhhh....!haina majotro kabisaa.
Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM/TV pichani kulia Wasi Wasi Mwambulambo akiwa na fundi mitambo, Dj Haroun wa Prime Time Promotions Ltd mchana huu ndani ya Uwanja wa Kambarage tayari kwa kulianzisha tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Ni Full kushangweka kama kawa wala haina majotro kwa wakazi wa Shinyanga.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya SBL mkoani Shinyanga wakijipanga vyema mikakati ya mauzo ya vinywaji vya kampuni hiyo kwa wateja wao.

0 comments:

Post a Comment