Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu akiwa na shada la maua muda mfupi baada ya kuwasili nchini
Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu akiwa katika pozi
Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu(kushoto)akipokewa na Maria Sarungi Muda Mfupi baada ya Kuwasili.
**************
**************
Mrembo
aliyeshinda taji la Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu ameshinda
taji la Miss Southern Afrika International 2011 katika mashindano
yaliyofanyika Ndola nchini Zambia na kushirikisha warembo kutoka nchi
mbalimbali za kusini na mashariki mwa Afrika.Nelly aliyepata mwaliko wa
kushiriki mashindano hayo kupitia bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
ameshinda taji hilo jumapili ya Juni 27 mwaka huu.
Fursa
hiyo imemsaidia Nelly kupata uzoefu kabla ya kwenda katika mashindano
ya Miss Universe kimataifa mwezi wa nane na tisa mwaka huu.Mashindano
hayo mbali ya kujenga mshikamano miongoni mwa nchi za kiafrika yanalenga
pia kuvutia na kutangaza utalii wa nchi washiriki.
Mbali
na kuhsiriki shindano la urembo,wakiwa nchini Zambia warembo washiriki
akiwemo Nelly walihsiriki na kufanya kazi mbalimbali za kijamii kama
vile kutembelea hospitali za watoto na vituo vya kulelea watoto na
kushiri maonyesho ya kimataifa ya biashara nchini humo.
Ukiondoa
Tanzania nchi nyingine za Afrika zilizoshiriki ni Namibia, Zambia,
Lesotho, Afrika ya Kusini, Botswana, Zimbabwe, Swaziland, Congo, Malawi
na Msumbiji.Nyota ya Nelly ilianza kung’ara pale aliposhinda taji la
Miss Universe katika shindano lililodhaminiwa na kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom Tanzania ikiwa ni sehemu ya azma ya kampuni hiyo ya
kuibua,kuendeleza na kulinda vipaji vya vijana wa kitanzania katika
sanaa na michezo.
Azma
hiyo inalenga kuwapatia fursa vijana ya kujiendeleza kimaisha kupitia
vipaji pamoja na kutimiza ndoto walizonazo katika sanaa.Kwa kushikilia
taji la Miss Southern Afrika Internation Nelly anawajibu wa kutoa elimu
kwa jamii juu ya saratani ya matiti na mfuko wa uzazi na atakuwa balozi
wa nia njema wa mtandao wa saratani ya matiti na mfuko wa uzazi Zambia.
Aidha
ushindi huo umempatia Nelly pamoja na zawadi mbalimbali mshahara wa
kwacha millioni moja kwa mwezi kwa kipindi cha miezi kumi na minne.
Kwa Hisani ya H@ki Ngowi.
Kwa Hisani ya H@ki Ngowi.
0 comments:
Post a Comment