SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 1, 2011

TOP MODEL FLAVIANA MATATA AZINDUA ‘FLAVIANA MATATA FOUNDATION!!


Mgeni rasmi  Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Mwansoko akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenela Mkangara wakati wa uzinduzi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION ambapo alimpongeza kwa kuonyesha kujali maendeleo ya mtoto wa kike hapa nchini na kuahidi kushirikiana naye bega kwa bega.

Mwanamitindo Flaviana Matata anayefanya kazi zake za uanamitindo katika jiji la New York nchini Marekani akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa  Taasisi yake inayoitwa FLAVIANA MATATA FOUNDATION itakayokuwa ikisaidia na kusomesha watoto wa kike wasiokuwa na wazazi au walezi (Yatima).

Taasisi hiyo ambayo itakuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia jamii hapa nchini akiwemo Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, Mwamvita Makamba pamoja na wadau wengine. Uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwamo Wabunge, Wafanyabiashara wakubwa pamoja na Viongozi wa Serikali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akieleza nia ya Flaviana Matata kuzindua Taasisi hiyo. Mwamvita Makamba ni mmoja wa wadau watakaokuwa wakisimamia taasisi hiyo pamoja wakishirikiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds FM Ruge Mutahaba.

0 comments:

Post a Comment