SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 31, 2011

Rais Jacob Zuma Na Kanali Gaddafi Wakiagana Baada Ya Mazungumzo

Rais Jacob Zuma na Kanali Gaddafi wakiagana baada ya mazungumzo.
Mazungumzo kati ya rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi yaliyofanyika mjini Tripoli yamemalizika bila ya kuwa na mwafaka wa maendeleo juu ya kusitishwa kwa vita nchini Libya.
Rais Zuma amesema Kanali Gaddafi anakubali kusitishwa kwa mashambulizi lakini hayuko tayari kuachia madaraka, kama inavyodaiwa na majeshi ya NATO na waasi wa Libya.
Pendekezo la kusitishwa kwa mashambulizi lilikataliwa mwezi uliopita wakati wa mpango wa upatanishi ulioendeshwa na rais Zuma kwa niaba ya umoja wa Afrika.
Msemaji wa waasi wa Libya amekataa wito wa kusitisha mapigano na kusema kuwa wao wataendelea na mashambulizi.

0 comments:

Post a Comment