SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 31, 2011

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI UGANDA AKABILIWA NA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA OFISI!!

Bw. Gilbert Bukenya
 Mahakama ya kudhibiti rushwa nchini Uganda imetoa hati ya uhalifu ya kumuita mahakamani aliyekuwa Makamu wa rais Gilbert Bukenya.
Hakimu Ngazi ya Kwanza Sarah Langa amewaita Bukenya pamoja na kampuni ya Motor Care Uganda Ltd kufika mahakamani mnamo Juni 6, 2011.
Bukenya anatakabiliwa na mashitaka katika sehemu mbili, ikiwemo la matumizi mabaya ya ofisi na tuhuma za kugushi zinazohusiana na kutolewa kwa mkataba wa kununua magari 80 aina ya BMW yaliyotumika wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM)uliofanyika nchini humo Novemba 2007.
Mkaguzi wa serikali aliyechunguza matumizi ya mkutano wa CHOGM amemtuhumu Bukenya kwa kushawishi kutolewa kwa tenda yenye thamani ya shilingi bilioni 9 kwa kampuni ya Motor Care Uganda Ltd kinyume na sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia manunuzi ya serikali nchini Uganda.
Mashitaka yanadai kuwa kati ya mwezi Mei na Novemba 2007, katika wilaya ya Kampala, Bukenya kinyume cha sheria aliagiza kufanyika manunuzi ya gari hizo.
Magari hayo 80 ya kifahari yalitumika kuwabeba wakuu wa nchi.
WAKATI HUO HUO
Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda kimeunda baraza kivuli la mawaziri litakalokuwa na jukumu la kuunda sera mbadala dhidi ya serikali.
Hata hivyo orodha ya mawaziri na wajumbe wa kamati za bunge za kambi hiyo ya upinzani, bado imebaki kuwa siri yao mpaka hapo kesho Juni Mosi.

0 comments:

Post a Comment