SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 31, 2011

WAANDAMANAJI 15 WAUAWA YEMEN!!

Watu 15 wameuawa nchini Yemen baada ya wanajeshi wanaomtii Rais Ali Abdullah Saleh kuwafyatulia risasi waandamanaji katika mji wa kusini wa Taiz.Taarifa kutoka katika hospitali zimesema huenda idadi hiyo ikaongezeka, na kwamba mamia ya watu hao wamejeruhiwa.
Vikosi vya polisi viliwafyatulia risasi, kupiga mabomu ya kutoa machozi na kutumia mabomba ya maji kuwatawanya waandamanaji nje ya jengo la halmashauri ya jiji.
Waandamanaji hao walikuwa wakidai mwenzao mmoja aliyekamatwa aachiwe huru.

0 comments:

Post a Comment