SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 1, 2011


BAADA YA ALBUM YA ALUTA KONTINUA, KAA TAYARI KWA JAYSCO DAGAMA.
Baada ya miaka kadhaa mtu mzima Prof Jay aka Dad katika mziki huu wa bongo fleva kukaa kimya sasa yupo tayari kuandaa album yake nyingine inayokwenda kwa jina la JAYSCO DAGAMA.
Prof Jay amesema ameamua kuiita album hiyo kwa jina la Jaysco Dagama kutokana na kukubali harakati za mtu mzima Vasco Dagama so na yeye anazifananisha harakati hizo kama zake katika mziki huu wa bongo fleva tokea alivyoanza game mpaka sasa heshima yake bado ipo pale pale.

Akiwa anatesa na wimbo wake mpya unaoitwa KAMA IPO ambao nao utakuwepo kwenye album Prof atarajia album hii mpya atafanya na wasanii kadhaa wa bongo fleva kama vile Mr. Nice, 20%, Dully Sykes na wengine wengi wale wenye mapenzi mazito na bongo fleva, na kuhusu studio amesema album hiyo itakuwa na studio tofauti tofauti so mashabiki wake mkae mkao wa kupata chakula cha ubongo kutoka kwa JAYSCO DAGAMA.
Credit to Dj Choka.

0 comments:

Post a Comment