SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 13, 2011

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE

Sehemu ya watanzania waishio New York na vitongoji vyake, wakianza kukusanyika kwa ajili ya kujiandaa kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa ajili ya kukutana na kuzungumza nao jana Juni 11, 2011.
Idd mtoto wa Kawe jijini Dar es Salaam (kulia) akijumuika na wadau wenzake katika hafla hiyo ya wabongo.
Katika hafla hiyo hata viongozi wa Jumuiya hiyo hawakuwa nyuma katika kutekeleza majukumu yao kama kawaida japo ilikuwa ni jumapili, hapa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Miriam Abu (kushoto) na Mweka hazina msaidizi, Mzee Temba, wakiwa na nyaraka zao ambapo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajiri Watanzania wapya waliokuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya hiyo.
Jumuiya hiyo ilianza kuwa active zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa kuiongoza uliofanyika mwezi April mwaka huu na kuwapata viongozi wapya kama Mwenyekiti, Haji Hamis na Makamu wake huyo, Katibu Vicent Mughwai na Katibu msaidizi, Shaban Mseba na Mweka Hazina,  Phillip Lwiza na msaidizi wake, Mzee temba na sasa Jumuiya hiyo imejipangia majukumu na malengo mengi ikiambatana na mikakati kabambe ya kuwawezesha kusonga mbele katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kusaidiana kimaisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake wakati alipokutana nao  kwa ajili ya mazungumzo nao na kuwatambua ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Pichani Juu na Chini; Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed gharib Bilal alipokuwa akiwahutubia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefiki 110.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo baada ya kuwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa jumuiya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimia na baadhi ya watanzania hao ikiwa ni sehemu  ya kuwaaga baada ya hotuba yake.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakhia Bilal akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya kinamama wanachama wa Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal akipiga picha za kumbukumbu.
Baadhi ya wabongo wakijisevia msosi wakati wa hafla hiyo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera Henri Rwekagingira (wa pili kushoto) akipozi na dada zake kwa picha wakati wa hafla hiyo.
Sufianimafoto pia alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo hapa akipozi na mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera Henri (wa pili kushoto) na dada zake. 
(Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment