SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, June 18, 2011

MAANDALIZI YA MAONYESHO YA SABA SABA YAPAMBA MOTO!!

Mkurugenzi  Mkuu wa Bodi ya Biashara ya Nje Ramdhan Hashim Khalfan akizungumzia maandalizi ya Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ambapo amesema yapo katika hatua za mwisho na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi rasmi tarehe 28 Juni, 2011.
Mkurugenzi  Mkuu wa Bodi ya Biashara ya Nje Ramdhan Hashim Khalfan akionyesha hatua za mwisho za ukarabati wa lango la kuingilia katika uwanja wa maonyesho ya Saba Saba ambapo amesema kwa mwaka huu siku uzinduzi Viingilio vitakuwa Sh. 3000 (wakubwa) na Sh. 1000 (watoto) wakati katika siku za kawaida za maonyesho hayo ni sh.2500 (wakubwa) na Sh.500 (watoto).
Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Masoko na Huduma Masha Hussein akionyesha waandishi wa habari moja ya mahema yatakayotumiwa na wafanya biashara katika maonyesho hayo ambapo amesema hema moja lina ukubwa wa Mita Mraba 1000 na uwezo wa kuingiza washiriki 60. Kushoto ni Afisa Mwandamizi Biashara za Nje Bw. Stephen Kobero.
Hema Kuu kutakapofanyikia uzinduzi rasmi wa maonyesho hayo.
Bustani iliyotengenezwa kitaalam kwa maua yaliyoandika maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam iliyopo nje ya uwanja huo.
(Picha na Geofrey Mwakibete wa Mo Blog).

0 comments:

Post a Comment