Hatari tupu Libya.
Waasi wa Libya wamedhibiti miji mitatu iliyo kwenye barabara inayoelekea mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Miji hiyo mitatu ipo katika njia panda muhimu, inayounganisha maeneo mbali mbali magharibi mwa Libya.
Nazo ndege za NATO pia zimeshambulia tena eneo lenye makazi ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Wakati
huo huo, Umoja wa Mataifa umeonywa na Umoja wa Afrika kuwa operesheni
ya kijeshi nchini Libya, imeanzisha “mfano wa hatari.”
Umoja
huo wa Afrika umetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ili zitafutwe njia
za kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment